Thursday, 28 November 2019

Wananchi wameshauriwa kuvifanyia tathimini ya kina Vyama vya Siasa nchini

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akiwahutubia Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa,Wilaya, Mabaraza ya jumuiya za CCM  Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ziara zake za kuimarisha Chama Zanzibar.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt.Bashiru Ally,akiweka jiwe la msingi katika Tawi la CCM Bandamaji Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
************************************
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
WANANCHI wameshauriwa kuvifanyia tathimini ya kina Vyama vya Siasa nchini vyenye usajili na vinavyopokea na ruzuku kisha kuchagua Chama chenye sifa na vigezo vya kuongoza nchi.
Wito huo ameutoa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Bashiru wakati akizungumza na Wana CCM na Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema Watanzania wanahitaji chama chenye nguvu, kitakachosimamia rasilimali za nchi,kitakacholinda mipaka ya nchi,kitakacholinda Mapinduzi,Muungano na Uhuru kama kinavyofanya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema  Vyama vya upinzani vya Tanzania sio madhubuti na havina uwezo wa kushindana na CCM kwani havipo karibu na wananchi vimekuwa vikiibuka wakati wa uchaguzi bila kuwa na sera wala muelekeo wa kiushindani katika medali za kisiasa.
Alisema CCM imejipambanua katika kuwahudumia wananchi kama kilivyoahidi katika kampeni zake zilizopita.
Katika maelezo yake Kkatibu mkuu alisema  chama hicho kimetengeneza fomu milioni moja kwa ajili ya uchaguzi wa ndani kuwashindanisha wana ccm kwa uchaguzi wa ndani ya chama kwa lengo la kupata wagombe bora na wenye sifa, upinzani waseme wao wamepitia mchakato upi kuwapata wagombea wao waonadai wameenguliwa kwa kuonewa..
Alisema chama cha mapinduzi CCM ndio chama pekee Nchini Tanzania chenye kufuata na kutoa demokrasia kuliko vyama vyengine vyote vya upinzani.
Alisema kwa msingi huo ndio maana chama hicho kinaendela kukubalika zaidi Tanzania katika kila kona.
Alisema ifike wakati lazima wananchi watambue hakuna chama kingine zaidi ya CCM  kitakachoendeleza na kusimamia misingi imara ya kulinda mapinduzi sambamba na kulinda Muungano.
Aidha katibu mkuu aliweka wazi kwamba tafsiri ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unatoa picha kuwa chama hicho kitashinda kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

No comments:

Post a comment