Happy Lazaro,Arusha.

Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto,Dokta
Faustine Ndungulile amesema baada ya tafiti kubaini tatizo la minyoo
ya TEGU ya nguruwe kuongezeka kwa kasi hapa nchini na kusababisha
athari za afya kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa kifafa

amewatahadharisha  walaji wa nyama hiyo kuhakikisha wanakula nyama
hiyo  na mbogamboga zilizopikwa vizuri.

Dokta Ndungulile ametoa tahadhari hiyo  leo jijini Arusha katika
mkutano wa  kwanza wa kimataifa unaofanyika katika bara la Afrika
ukiongelea minyoo ya tegu ya nguruwe kwa lengo la kuweka mikakati ya
pamoja ni jinsi gani nchi hizo zinaweza kutokomeza ugonjwa wa minyoo
ya Tegu ya Nguruwe.

Amesema ulaji wa nyama ya nguruwe ambayo ina minyoo ya Tegu ya Nguruwe
au mayai,au   mbogamboga ambazo zimebeba mayai yaliyotokana na kinyesi
cha nguruwe au binadamu ambae ana minyoo tumboni na zikawa hazijapikwa
vizuri zinaweza kupelekea magonjwa ya afya ikiwemo kifafa ambacho
hupelekea kifo.

Amesema kuwa,athari zinazoweza kupatikana katika mnyama huyu ni kubwa
ikiwemo kupata ugonjwa Wa kifafa , na tatizo hili limeshaingia katika
nchi yetu na limeanza kuathiri zaidi katika mikoa ya Manyara,Njombe,
Mbeya ,Sogwe ,Mbeya pamoja na mkoa Wa Arusha na asilimia 16%ya
wananchi wanaoishi mikoa hii wameshaathirika na ugonjwa huu.

Amebainisha kuwa, hadi sasa serikali yetu haijapata chanjo kwa ajili
ya kumzuia mnyoo huyo wa nguruwe na ipo katika utafiti wa kuangalia
namna ya kumdhibiti,lakini pia tunaweza kuzuia  kwa kuakikisha kuwa
tunafuga bila mifugo yetu kuzagaa,pia kwa wale tunaochinja tuhakikishe
tumewapima mifugo yetu kwanza bila ya kuwachinja.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya magonjwa ya binadamu nchini NIMRI
,Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa,kwa hapa nchini wanatekeleza mradi
huo kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kilimo cha sokoine SUA ambao
lengo lake kubwa ni kupata taarifa za kutosha kuhusu tatizo la ugonjwa
unaosababishwa na minyoo ya Tegu inayopatikana kwa mnyama nguruwe.

“mradi huu unatekelezwa na nchi zingine mbili afrika ambazo ni
Mozambiq pamoja Zambia  na tunashirikiana na wadau wetu wa utafiti wa
ujerumani kutoka chuo kikuu cha  Munchen  ,mradi huu umetuwezesha
kununuavifaa vya maabara kwa ajili ya kuweza kufanya utafiti wetu
vizuri kwa kiwangoncha juu ,pia umetusaidia kuwapeleka vijana wetu
kwenda kupata elimu  katika shaghada zauthamini PHD, lakini mradi huu
umetuleta pamoja nchi hizi za Afrika  na lengo kubwa ikiwa  ni
kutokomeza au kuzuia watu wasipate ugonjwa huu unaotokana na minyoo
hii ya Tegu ”amesema.



 Naye Kaimu mkuu wa idara ya tiba ya mifugo na afya ya jamii ambaye
pia ni mkurugenzi wa mtandao wa utafiti wa kisayansi  Prof,Helena
Ngowi  amesema kuwa ,mnyoo ni hatari sana kwa sababu anaweza kuleta
athari kubwa katika utumbo wa binadamu hadi katika ubongo wa binadamu
,anaamini bila ya kuwa na mfugo alie athirika binadamu hawezi kupata
ugonjwa huu,pia tafiti hizi zilianza kufanyika tangu mwaka 199 na bado
zinaendelea  na kiwango cha tatizo kimeshajulikana ,tunashirikiana kwa
lengo la kushirikiana katika kupambana na tatizo hili kwa sababu
hazina mipaka ,kwa ivyo tunavyoshirikiana na nchi hizi zingine
tunaweza kutokomeza kabisa tatizo hili pia tutashirikisha jamii ili
tuweze kutokomeza.

mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: