Saturday, 9 November 2019

MWENYEKITI WA UVCCM (M) RUVUMA COMREDI RAYMUND MHENGA KUWARIPOTI KWA RAIS MAGUFULI WATUMISHI WA SERIKALI WALA RUSHWAMwenyekiti huyo wa Uvccm ameyasema hayo leo kwenye mahafali ya 10 ya Wahitimu wa Chuo Cha Ufundi Top One College.Mhenga amesema anapeleka majina ya watumishi wa Serikali  ambao wanakwamisha wawekezaji na mabingwa wa Kuomba Rushwa kwa wananchi kwa Rais Magufuli kupitia kwa Mkuu wa Mkoa,maana hali hiyo ya watumishi kupenda Rushwa inachelewesha maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma.

"Hawa wapenda Rushwa ndio wanaochelewesha maendeleo ya Mkoa wetu na wanawaumiza wananchi wetu na wanatupa wakati mgumu chama chetu kuaminiwa na wanamchonganisha Rais Magufuli na Serikali yake kwa Wananchi"

Mwenyekiti pia aliwaeleza wahitimu wa chuo hicho namna bora za kujiajiri na kwamba serikali imetoa fursa nyingi za uwezeshaji kwa Vijana hasa za Mikopo kwenye Vijana wenye ujuzi hivyo wasisubiri tu ajira ila wajiunge vikundi hili kupatiwa Mikopo na kuwa kama sehemu ya mtaji kutimiza malengo yao.

No comments:

Post a Comment