Na Ferdinand Shayo,Killimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Siha  Onesmo Buswelu  amemuonya Mkanadarasi wa kampuni ya Rural and Urban Contractor  anayetekeleza Mradi wa umeme vijijini REA katika  Kijiji cha wiri kata ya gararagua kwa  kutoweka nguzo katika baadhi ya vijiji  huku vingine akiviruka na kusababisha malalamiko kwa wananchi ambao ni walengwa wa mradi huo.

Amemtaka Mkandarasi huyo kufika eneo la kijiji cha Wiri  kata ya Gararagua na kuhakikisha kuwa wananchi wanaunganishiwa umeme na emdapo atakiuka agizo hilo hatua zitachukuliwa dhidi yake.

Mkuu huyo wa Wilaya alifanya ziara ya kutembelea kijiji hicho na kuangalia maendeleo ya mradi wa kuwaunganisha wananchi na mradi wa umeme vijijini ambapo alikutana na malalamiko ya wananchi wakilalamikia mkandarasi huyo kuleta nguzo na kuzichukua kuzipeleka katika kijiji kingine badala ya kuziweka katika kijiji hicho ndipo alipoamua kumpigia simu Mkandarasi huyo na kumpa maelekezo.

"Wananchi wote fanyeni maandalizi katika nyumba zenu ili muweze kuunganishiwa umeme ni haki yenu,Mheshimiwa Raisi kasema Muunganishiwe Umeme ,Waziri wanishati pia kasema nani wa kupinga hapa nataka umeme mpaka disemba watu wawe wamepata umeme kama ilivyo adhama ya serikali"

Akizungumza kwa njia ya Simu Mkandarasi huyo Zuberi Ismail  amekiri kupokea maagizo hayo ya Mkuu wa Wilaya na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja.

Mwenyekiti wa Kitongoji  Fares Mmariamesema iwapo wananchi hao wataunganishiwa umeme wataondokana na adha ya kukosa umeme iliyowakabili kwa miaka mingi iliyopita.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: