Monday, 11 November 2019

MBUNGE MALEMBEKA AWATAKA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI


NA HERI SHAABAN(ZANZIBAR

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa Kaskazini Unguja, Angelina Malembeka(CCM) amewataka Wanawake wa Mkoa huo kujikwamua kiuchumi na kuacha maisha tegemezi.

Malembeka aliyasema hayo katika mafunzo endelevu ya  Wanawake na Vijana yalioandaliwa na ofisi ya Mbunge, ambayo yalikuwa yakitolewa bure katika  ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini.


"Wanawake wa Kaskazini Unguja mafunzo haya ni endelevu ya Wajasiriamali kwa Wanawake na Vijana kwa mwaka nawapatia elimu mara mbili kwa ajili ya kuwajengea maarifa na  wawe wajasiriamali bora ili waweze  kukuza masoko"alisema Malembeka.


Mhe. Malembeka alisema "dhumuni la mafunzo haya ni kuwapa mikakati kila mshiriki wa mafunzo aweze kumiliki Kiwanda kwa ajili ya kukuza uchumi.

Malembeka alisema    katika mafunzo hayo Wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wamepatiwa elimu ya Kutengeneza mifuko Mbadala ,sabuni ya maji,sabuni ya unga,sabuni ya kuoshea  nywele (shampoo)dawa ya kuondoa madoa katika nguo,dawa ya kusafishia madirisha ya vioo

Pia aliwataka watumie elimu ya ujasiriamali kwa kubuni viwanda vidogo vidogo vitakavyowakomboa wanawake na vijana katika Mkoa wa Kaskazini Unguja katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Awali  Malembeka alishatoa elimu kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja jinsi ya utengenezaji wa Chaki , mishumaa, batik, vikoi elimu ya mikopo na elimu ya ujasiriamali, aidha amewakabidhi mashine za kutengezea chaki tatu, mashine nne za kutengeneza matofali na jmashine kumi za kutengeza mishumaa zote amewawezesha  Wanawake na vijana .

Pia alitoa vitanda 10 vya kisasa vya kujifungulia katika  hospital zilizopo  Mkoa wa Kaskazini Unguja

"Katika Mkoa huu  tayari nimewaunganisha Wanawake na Vijana kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya Tano Dkt. John Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt.Ally Mohamed Shein katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda na Kauli mbiu yetu "*Mkoa wangu Kiwanda changu"* alisema.

Kwa upande wake James Obasanjo Mwalimu wa mafunzo aliwataka viongozi wengine kuiga mfano kama wa  Mbunge Malembeka anavyowawezesha wanawake na vijana kuwatafutia fursa ambazo zitawafanya wananchi kuwa na miradi yao mikubwa.

"Ili uweze ufanikiwe ujasiriamali ni kujituma   na kuchukua hatua nawaomba wajasiriamali wote mafunzo haya mliopata leo (jana)iwe chachu kwenu muweze kusonga mbele kwa kutengeneza vifungashio bora, baada serikali yetu kuondoa mifuko ya rambo sasa zamu ya mifuko ya karatasi "alisema Obasanjo

Naye mgeni rasmi Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (MNEC)Abeid  Mohamed Khamis alisema wakati wa Kampeni bado, amewaomba akina Mama muache kubeba wagombea, waacheni Waliopo madarakani wafanye kazi zao,muda ukifika mtafanya kampeni.

No comments:

Post a comment