Friday, 15 November 2019

MANISPAA YA LINDI KUTENGA BILIONI 4 KWA AJILI YA KUJENGA SOKO LA KISASA


Afisa mradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Equality for Growth (EfG) , Susan Sitta akimkabidhi mfuko wenye machapisho mbalimbali , Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge.
Afisa Utawala wa shirika hilo la EfG,  Eva Buhemba, akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge  (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  Wanawake wajasiriamali kutoka  katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG ambao wapo katika ziara ya kuwahamasisha wanawake wafanyabiashara masokoni wa  mkoa huo kujiunga katika umoja wa kitaifa.
Na Mwandishi Wetu, Lindi.
HALMASHAURI Manispaa ya Lindi mkoani hapa inatarajia kutumia sh. Bil.4 kwajili ya kujenga soko la kisasa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Lindi,  Joumary Satura ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG), kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Lindi, alisema kuwa ukamilikaji wa soko hilo litaweza  kuwanyanyua kina mama wajasiriamali ambapo kwa sasa bado wanatumia soko la zamani ambalo ndilo linatakiwa kubomolewa.
Aidha alisema kwamba licha ya ujenzi wa soko hilo jipya ambalo litakuwa la ghorofa moja ramani na michoro kadhaa ilishakamilika.
Satura alisema fedha hizo zitatokana na vyanzo vya ndani na serikali kuu na taasisi za kifedha benki taratibu mbalimbali zinafanyika.
Aliongeza kwa kusema kuwa hivi sasa miundo mbinu ya soko hilo la zamani sio mizuri kutokana na idadi ya watu wanaongezeka.
Alisema kwamba kwa hiyo ukamilikaji wa soko hilo itawezesha makundi mbalimbali kutumia fursa hiyo hasa wale akina mama wajasiriamali wanaochuuza samaki mbogamboga watanufaika.
Hata hivyo aliwaambia viongozi hao kuwa makundi yanayokopeshwa fedha hasa hivi vikundi vya uzalishaji mali huwa wagumu kurudisha deni.
Mpaka sasa ni zaidi ya shs mil.200 zilishakopeshwa kwa vikundi vya uzalishaji mali lakini  mpaka mwaka huu havijarudisha deni hilo tangu miaka 2014 hadi 2019.
Naye Afisa Utawala wa shirika hilo la EfG,  Eva Buhemba alisema madhumuni wa shirika hilo kuwakutanisha kina mama wajasiriamali kuwa na sauti moja katika masoko.
Ambapo wanaonekana wanakuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji, kumiliki vizimba wanakuwa watu wanaohangaika hata biashara yenyewe anayoifanya jkwa siku anapata shs 7,000 tu.
Buhemba alisema hata kuwa na sifa ya kukopesheka huwa hawana kwani hata kizimba chenyewe alishakodi inabidi alipe, miliki huwa wanaume.
Alisema hata hivyo uongozi wa soko huwa kina baba sio wanawake ni wachache mno kwahiyo shirika huwa linawezesha kuwapa elimu kina mama.
Aliongeza kwa kusema kwamba mpaka sasa shirika linafanya kazi katika mikoa tisa nayo ni Mtwara, Lindi, Mbeya, Iringa, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam katika halmashauri ya manispaa ya Ilala na Temeke.

No comments:

Post a Comment