Monday, 11 November 2019

ARUSHA KUMEWAKA MOTO,MAJANGILI SUGU NA MATAPELI WA MITANDAO,MIKONONI MWA RPC SHANA,PASIPO KUFURUKUTA.

Na Lucas Myovela_Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewashikilia majangili wawili sugu wa uwindaji haramu wa wanyamapori pamoja na bunduki mbili za kivita na risasi 15,huku majangili wengine wamekatwa na nyama za twiga.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,ACP JONATHAN SHANA,Amesema majangili hao wamekamatwa wilayani Loliondo wakiwa na bunduki mbili za kivita,hukumbunduki zilizo kamatwa ni Ak47 pamoja na G3.

"Jeshi la Polisi kwa kishirikana na kikosi labambe cha kuzuia ujangili kanda ya kaskazini imewakamata imekamata bunduki mbili zilizo kuwa zinatumiwa na majangili sugu na mmoja wao baada ya majibishano ya risasi tunahisi ametangulia mbele za haki baada ya kupigwa risasi na kuvuja damu nyingi na wengine wawili kukimbia nchi jorani na kuacha siraha hizo, siraha hizo ni AK47 yenye namba 174364 ikiwa na risasi 6,pia bunduki nyingine ni G3 yenye namba A36011858 ikiwa na risasi 9,siraha hizi zimekatwa eneo la Naani,tarafa ya Loliondo,mpaka wa Tanzania na Kenya".Alisema ACP SHANA.

KUKAMATWA KWA MAJANGILI HARAMU WA WANYAMA PORI.

Aidha jeshi la Polisi limewshikilia watu wawili wilani Ngorongoro waliofahamka kwa majina  ya Nyamahanga Mwita (19) na Chacha Marwa (20),ambao wote ni wakazi wa wilayani Serengeti mkoani Mara,wote hawa walikuwa wanafanya shughuli haramu za uwindaji katika hifadhi ya pori tengefu la Loliondo wilayani Ngorongoro.

"Watu hawa wamekematwa wakiwa ndani ya pori wakiwa waanika nyama kwaajili ya kusafirisha na kuzikata vipande vipande mbali na nyama hizo pia walikuwa mapanga,pikipiki mbili,sime pamoja na Nyaya za kutegea wanyama".Alisema ACP Shana.

KUKAMATWA KWA NYARA ZA SERIKALI.

Kamanda Shana ameweka wazi pia kuwashikalia watu watano wakazi wa wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara,Kwa kukutwa na Meno mawili ya Tembo kinyume cha sheria.

KATIKA TUKIO LA KIUTAPELI KUTUMIA JINA LA GAVANA WA BANK KUU (B.O.T)

Katika tukio la kitapeli lisilo la kawaida kwa njia ya mtandao tukio hilo linalo muhusisha kijana mmoja aliye fahamika kwa jina la Aman Gabriel Mbise (32),mkazi wa Maji ya Chai wilayani Arumeru, aliye kuwa akijifanya ni Gana wa Bank kuu ya Tanzania,na kutumia jina la Gavana Prof.Florence Luoga,katika mtandao wa facebook na kuwatapeli wananchi,Pia jeshi la polisi nimemtia nguvu ni aliyekuwa wakala wa Juma Hussein Yahaya (33),aliyekuwa anasajili laini hizo za utapeli.

"Baada ya kupata taarifa hizo tulianza kufuatilia tulingundua mtandao huo wa facebook ulifunguliwa kwa namba ya simu 0785349763 ambayo katika usajili wake walitumia kitambulisho cha Norrish Andrew James,ambaye ni raia wa Australia aliyefika hapa nchini na kutaka kupata namba za Tanzania ndipo matapele hao wakaamua kusajili laini mbili pamoja na yao kwa ajili ya utapeli kwa kutumia kitambulisho cha raia huyo wa kigeni na Tapeli huyu anajenga jumba la kifahari sana kwa pesa za wizi".Alisema ACPA Shana.
 Nyumba inayodaiwa kujengwa na mtuhumiwa wa wizi wa mtandaoni Aman Gabriel Mbise.

Kupita mahojiano ya jeshi la polisi na mtuhumiwa wa utapeli Aman Mbise,jeshi la polisi limebaini mtuhumiwa anajenga jumba la kifahari huko Maji ya Chai,Wilayani Arumeru,kupitia pesa za utapeli kwa kujifanya yeye ni Gavana wa Bank Kuu ya Tanzania na kuahidi kuwapa kazi watanzania.

Kamanda Shana ameendelea kutoa wito kwa watanzania wote kutokutuma fedha lwa watu wasiyo wafahamu ili kuepeka kuendelea kuibiwa kila siku.

No comments:

Post a comment