Monday, 14 October 2019

WASTAAFU WASHAURIWA KUFUGA SAMAKI


 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (kulia) akizungumza alipotembelea banda la ufugaji wa samaki katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida. Wa pili kulia ni Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi mfugaji mkubwa wa samaki mkoani Singida.
 Wafanyakazi wa Mzee Juma Mkhofoi wakiyafanyia usafi mabwawa ya ufugaji wa samaki yanayomilikiwa na mzee huyo.


Mzee Mkhofoi (kulia) akiwa katika banda la kufugia samaki kwenye maonesho hayo. Samaki hao wametoka katika moja ya mabwawa yake.
Mfugaji Mzee Mkhofoi akiangalia kibao cha tarehe aliyopandikiza vifaranga vya samaki katika bwawa hilo.
Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi (wa pili kulia) akielekeza wananchi jinsi ya ufugaji samaki katika maonesho hayo.

 Hapa akiwapa samaki chakula.
 Mzee Mkhofoi akitoka kwenye ofisi ya mda iliyopo kwenye mabwawa yake ya samaki.
 Usafi kwenye mabwawa hayo ukiendelea.
 Usafi kwenye mabwawa hayo ukiendelea.Na Dotto Mwaibale, Singida

WASTAAFU wameshauriwa kufuga samaki ili waweze kupata chakula chenye lishe bora na kuinuka kiuchumi badala ya kutegemea fedha za kiinua mgongo pekee.

Wito huo umetolewa na Juma  Ikhofoi mfugaji mkubwa wa samani  mkoani Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika Uwanja wa Bombadia mjini hapa.

" Niwaombe wastaafu wenzangu wasikae bure na kutegemea kiinua mgongo pekee kuendesha maisha yao bali wafuge samaki kwani watapata kitoweo chenye lishe bora na fedha za kujikimu  " alisema Mkhofoi.

Mkhofoi alisema gharama za ufugaji wa samaki ni ndogo  na soko lake ni kubwa tofauti na kilimo ambacho kinahitaji mambo mengi.

Aliongeza kuwa mabwawa ya samaki yanaweza kuchimbwa eneo lolote na chakula chao ni pumba ya mpunga na mahindi ambayo haizidi sh. 5000 kwa gunia na udavi ni sh.250,000 ambapo 
samaki kwa bwawa moja kwa siku wanakula kilo moja tu.

Alisema yeye baada ya kustaafu Wizara ya Maji na Umwagiliaji aliamua kuchimba mabwawa 67 kwa ajili ya kufuga samaki ambapo kila bwawa alitumia sh. milioni moja na sasa anafurahia 
ufugaji huo.

Alisema mabwawa hayo aliyachimba mwaka jana na sasa ameanza kupata matunda ya ufugaji huo kwani kuanzia mwaka jana mwishoni hadi mwaka huu mwanzoni ameweza kupata zaidi ya 
sh.milioni sita baada ya kuvua samaki  na kuwauza.

" Nimeanza kupata pesa kwa kuwauza samaki aina ya sato ninaowafuga pamoja na kitoweo chenye lishe ambacho kinakubalika kwa afya tofauti na nyama zingine " alisema Mkhofoi.

Mkhofoi alisema lengo lake ni kuwa na mabwawa zaidi ya 80 na kila wiki awe ana zalisha kilo kuanzia 1000 hadi 2000 na kuwa soko lake kubwa litakuwa hapa hapa mkoani Singida na 
hapendi kuwauzia wafanyabiashara kwa kuwa wanaenda kuwalangua walaji ambao watashindwa kupata chakula chenye lishe bora.

Mkhofoi ametumia fursa hiyo ya maonesho hayo kuwaomba wananchi wa mkoa wa Singida ambao watahitaji kupata mbegu ya samaki hao kwa ajili ya kufuga na kwa  kitoweo  kwa ajili ya 
matumizi ya nyumbani wawasiliane naye kwa namba ya simu 0755 735441 na 0655 735441.

No comments:

Post a comment