Happy Lazaro,Arusha

Wadau wa Mitandao Nchini wameaswa kuzingatia Matumizi sahihi ya Mtandao na kuepuka matumizi hatarishi ili kuweza kuchochea maendeleo endelevu katika teknolojia ya Tehama.

Akiongea katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa jukwaa la Uongozi na utawala wa mitandao Nchini( IGF ),Mkuu wa Chuo cha uhasibu Arusha ,Frof.Eliamani Sedoyeka amesema ipo haya kwa serikali kuweka mazingira shirikishi katika matumizi sahihi ya mitandao.

Prof,Sedoyeka ambaye pia ni Mdau wa Tehama,amesema hakuna haki ya matumizi ya mitandao isiyoendana na wajibu ukizingatia matumizi holela ya mtandao kwa taarifa zisizo za kweli jambo linalosababisha usumbufu na hatarishi.

"Kuna taasisi nyingi wakati mitandao inaingia Nchini ziliingiwa na hofu na kupiga marufuku matumizi ya Mtandao ila kwa sasa zimeelewa umuhimu wa teknolojia ya mitandao" Amesema

Naye mratibu wa jukwaa la uongozi na utawala wa Mitandao, Nazar Nicholas amesema mkutano huo umewaleta wadau wote wa mitandao, zikiwemo asasi za kiraia,mamlaka ya mawasiliano Tanzania na wataalamu wa mitandao kwa lengo la kujadili matumizi sahihi ya Mtandao ikiwemo usalama wa taarifa Mtandaoni.

Alisema kuwa,mkutano  huo umewaleta wadau wote wa maendeleo kwa ajili ya kuzungumzia maswala yanayohusu usalama wa watoto Mtandaoni,na taarifa za watu.

Alisema kuwa changamoto kubwa watu wamekuwa wakitumia mitandao vibaya ,matumizi ambayo hayapo sahihi ,hivyo kuna haja kubwa ya kuelimisha watu juu ya matumizi yaliyozingatia maadili.

Aidha aliwataka vijana wazazi kuangalia namna ya kutumia mitandao  kwa ajili ya matumizi endelevu na ambayo yanaweza kusaidia kuleta tija katika maisha yetu na kusaidia watoto wetu,hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanaangalia taarifa  zitaleta athari  gani kwa wengine.

Naye mmoja wa watoa mada ambaye ni mkurugenzi wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC)Abubakar Karsan alisema kuwa,mitandao imekuwa na faida kubwa katika kuchochiea maendeleo ikiwemo kwa wanahabari kupeleka taarifa zao kupitia rasilimali Mtandao.

Karsan alisema kuwa, mitandao imekuwa ikitumika kwa ajili ya afya, elimu na utawala bora ,hivyo alitoa rai kwa serikali kupeleka mitandao nchi nzima na wananchi kuweza kuupata kwa bei nafuu na hatimaye kuweka maendeleo.

Hata hivyo akitaka kutolewa elimu kwa njia ya  Mtandao ili watu waweze kufanya shughuli zao na hatimaye  rasilimali Mtandao kuweza kupunguza gharama za maisha.

Ends...
Share To:

msumbanews

Post A Comment: