NA HERI SHAABAN

NAIBU Meya wa halmashauri ya Ilala Ojambi Masaburi, amewataka wafanyabiashara wa manispaa Ilala  kulipa kodi ili serikali iweze kupata fedha katika sekta ya elimu.

Naibu Meya Masaburi aliyasema hayo leo katika mahafali ya 15 ya shule ya  sekondari Juhudi Wilayani Ilala.

"Mimi kama Naibu wa wilaya ya Ilala tunaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli mpango wa elimu bure pia nawakumbusha wafanyabiashara wote wa Ilala kulipa kodi kwa wakati ili Serikali iweze kupata fedha kwa ajili ya huduma za jamii ikiwemo sekta ya elimu" alisema Masaburi.

Masaburi alisema serikali ya awamu ya tano inaimiza mkakati wa elimu bila malipo hivyo katika kuunga mkono juhudi za serikali amewashauri wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili fedha zitumike katika masuala ya elimu.

Aidha aliwataka wadau wa elimu kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchangia mpango wa elimu bila malipo.

Katika mahafali hayo ya 15 Masaburi amesema Novemba  Mosi mwaka huu atakarabati shule ya juhudi kutokana na shule hiyo kuwa chakavu.

Amewapongeza  wanafunzi wa shule ya Juhudi kwa mafanikio mazuri kitaaluma na amewataka kuwa na nidhamu wakati wote ikiwemo kuwaheshimu walimu pamoja na Wazazi.

Pia aliwataka wazazi wa wilaya ya Ilala ambao wanasomesha  kufatilia maendeleo ya watoto wao na kuweka utaratibu wa kukagua daftari kila wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Joseph Deo alisema  mahafali hayo ya 15 katika shule hiyo  jumla ya wanafunzi 400 wamemaĺiza kidato cha nne ,shule  ina jumla ya wanafunzi 1937 Walimu 96 kati yao wa kike 63 wa kiume 33 watumishi wa kawaida sita.

Deo alisema kitaaluma mafanikio ya shule imeweza kufanya vizuri mwaka hadi mwaka kwa kidato cha pili mwaka 2017.jumla ya wanafunzi 445 wamefaulu 419wamefeli 19 sawa na asilimia 94,2018 jumla ya wanafunzi 364wamefaulu,340wamefeli 11 sawa na asilimia 96.

Akielezea mafanikio ya shule hiyo kwa mkoa wa Dar es salaam imeshika nafasi 16 kiserikali nafasi ya pili.

MWISHO
Share To:

msumbanews

Post A Comment: