Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dokta.Harrison Mwakyembe
amewataka watanzania kuacha tabia ya kudharau ,ngozi zao nyeusi kwa
kujichubua ili wawe weupe huku akiwasihi kuacha  kuvaa nywele bandia
ambapo amesema huo ni ulimbukeni na ujinga na badala yake wanatakiwa
kuenzi utamaduni wa Afrika.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo  leo Oktoba 25,2019 jijini Dodoma
wakati akifungua Mashindano ya Tamasha la Urithi Festival ambapo
amesema ulimwengu wa leo kuna baadhi ya Watanzania wamekuwa wakidharau
ngozi yao nyeusi kwa kujichubua pamoja na kuweka nywele bandia ambapo
amesema vitendo hivyo ni ujinga ambapo amesema lengo la tamasha hilo
ni kupinga ukoloni na kuenzi utamaduni wa Kiafrika.

“Leo hii mtu anaona   ngozi nyeusi anajichubua ,huo ni ujinga ,unakuta
mtu ananunua nywele bandia [wigi],Mungu aliumba kwa maana yake ,nywele
za Afrika hata zikinyeshewa mvua ubora wake unabaki vilevile
haziharibiki  halafu wewe unakuja kudharau ,ngozi yetu ya kiafrika
halafu kuna mjinga Fulani anaanza kuiharibu ili iwe nyeupe huo ni
ujinga na utumwa.Waafrika tuna ngozi imara inayovumilia hali yoyote
ile lakini hatujitambui tu,Leo hii wazungu wameamka mapema
wanatutengenezea madawa ya kujichubua ngozi zetu ili waingize
pesa”amesema.

Aidha,Dokta Mwakyembe amesema mkoa wa Dodoma ni moja ya kituo kikubwa
cha utalii ambapo amewasihi watanzania kutembelea mkoa huo huku
akisema kuwa ni mkoa wa pekee Duniani ambao huzalisha zao la zabibu
mara mbili kuliko sehemu yoyote ulimwenguni.

Hata hivyo,Dokta Mwakyembe amesema tamasha la Urithi Festival tangu
lizinduliwe mwaka jana na Makamu wa Rais ,Mama Samia Suluhu Hassan
limekuwa na hamasa kubwa kwa nchi za Afrika Mashiriki ambapo
waliotembelea mabanda ni watu zaidi ya 1000 na waliofikiwa kupitia
runinga ni watu bilioni 94.

Katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda  amesema
utamaduni una sura pana  huku akishukuru mkoa wa Dodoma kwa kuandaa
tamasha hilo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge amesema amesema
tukio la Urithi Festival ni la kihistoria katika kukuza mnyororo wa
thamani wa zao la zabibu,huku pia akisema kuwa mkoa wa Dodoma ni mkoa
wa pekee ambapo kila kijiji kina vikundi vya ngoma za asili  na ngoma
hizo zikiendelezwa itasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
Umasikini.

Hata ,Dokta Mahenge amesema Tanzania inayo  fursa ya kuendelea kuenzi
lugha ya Kiswahili katika mapinduzi ya viwanda na kuongeza kuwa
Kiswahili ni nguzo muhimu katika Siri na maendeleo ya Teknolojia.

“Una jua nyenzo kubwa ya wachina kuimarisha teknolojia yao ni
kuithamin lugha ya kichina ,hivyo na Tanzania ina fursa kubwa ya
kuenzi lugha Kiswahili maana hata teknolojia tutazokuwa tunavumbua
mataifa mengine ni vigumu kutafsiri lugha moja hadi nyingine lazima
kuna maneno tutayapunguza kama siri ya teknolojia”.amesema.


Mashindano ya tamasha la  Urithi Festival yameanza rasmi leo Oktoba
,25,2019  na yanatarajia  kuhitimishwa Siku ya Jumapili Oktoba
27,2019.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: