Sunday, 27 October 2019

ILALA INAANZA UKAGUZI WA LESENI ZA BIASHARA


NA HERI SHAABAN

HALMASHAURI ya Ilala inatarajia kufanya ukaguzi wa leseni kwa wafanyabiashara wa manispaa ya Ilala.

Ukaguzi huo wa leseni unatarajia kuanza mwezi Novemba mwaka huu kata zote 36 wananachi wasio na leseni za biashara wametakiwa kulipa ili kuondoa usumbufu .

Akizungumza na waandishi wa habari manispaa ya Ilala leo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri alisema ukaguzi huo wa leseni kwa wafanyabiashara unatarajia kuanza hivi karibuni.


"Kuanzia Octoba Mosi Manispaa yangu ya Ilala maombi ya leseni yote ya leseni za biashara waombaji wanatakiwa kuomba kwa njia ya mtandao  waombaji  wataomba leseni ya biashara kwa kuingia na kusajili katika ukurasa wa mtandao  www.business .go.tz"alisema Shauri.


Shauri aliwataka wafanyabiashara wa manispaa hiyo ambao hawana leseni za biashara kufika Ofisi ya Arnatogluo Wilayani Ilala.


Aidha Shauri alisema katika kuboresha huduma za kisasa manispaa ya Ilala imesogeza huduma zake kwa sio na leseni za Biashara wameshauriwa wafike katika vituo vya Kata ambazo huduma hizo zinatolewa .

Mkurugenzi Shauri alizitaja kata hizo ni Tabata ,Buguruni,Vingunguti,Ukonga ,Tabata Liwiti na Chanika.


MWISHO

No comments:

Post a comment