MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na Kikosi kazi cha kuratibu na kusimamia miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa benki ya Dunia ambao walifika wilayani humo kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akisisitiza jambo wakati wa mamzungumzo hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa amekutana
na kufanya mazungumzo na Kikosi kazi cha kuratibu na kusimamia miradi
inayotekelezwa kupitia mkopo wa benki ya Dunia ambao walifika wilayani humo
kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.
Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwake, Afisa wa
Kujenga Uwezo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Debora Mkwemwa alisema kwamba
wamefika wilayani humo kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.
Alisema ufuatiliaji huo ni miradi ya ujenzi wa
barabara tatu,ujenzi wa soko ambao
tayari umekwisha na stendi kubwa ya mabasi Korogwe ambayo imekamilika na inatumika kwa sasa hivyo
kazi wanayoifanya ni kutaka kuangalia je wana Korogwe kupitia halmashauri na
viongozi wanaipokeaji hiyo miradi na wanaisimamia vipi ili waweze kuwahudumia
wananchi muda mrefu.
Alisema kwamba pia watawashauri namna ya kuisimami
miradi hiyo ikiwemo pia kushauriana kuhusu miradi watakayoipendekeza kwa ajili
ya siku zijazo baada ya kukamilika miradi ambayo walioichagua wenyewe huku
akieleza wakipata nafasi watapata miradi mingine inayoanza 2020-2021.
Afisa huyo alisema kwamba watashauriana nao
kuhusua na miradi watakaokuwa wameichagua ili iweze kuwa miradi rafiki ya kutoa
huduma na pia kuwanufaisha wana Korogwe.
Awali akizungumza baada ya mazungumzo hayo Mkuu
wa wilaya ya Korogwe Kissa alisema kwamba kama kuna hitaji matokeo ya haraka
sana inapaswa wawe wanaweka kwenye jamii ambayo itakuwa inanufaika zaidi
Alisema kwamba amelichukua suala hilo na atakwenda
kulifanyia kazi hasa kwaHalmashauri watu wa mipango na wachumi ambao ndio
wanaibuni hiyo miradi huku akiwashukuru wao kutaka kushirikiana na viongozi hao
ili fedha za miradi zisirudi na yeye kama DC ametambua kwamba huo ni uzalendo mkubwa kwani kufuatilia jambo
ndio mambo yanakwenda hivyo aliwashukuru sana kwa kuwa wamefanya shirikishi
hivyo kwa pamoja tutatoka na kitu kimoja.
Mwisho.
Post A Comment: