Thursday, 12 September 2019

Zuio La Kuendelea Na Masomo Kwa Wanafunzi Wajawazito Lasaidia Kupunguza Matukio Ya Mimba Shuleni

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Zuio la kuendelea na masomo kwa wanafunzi wanaobebeshwa ujauzito wakiwa shuleni linatajwa kusaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza matukio ya mimba kwa wanafunzi katika meneo mengi Nchini.

Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh.   William  Ole Nasha ameyabainisha hayo  Bungeni Jijin Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Mh. Aida Joesph Kenan aliehoji juu ya matamko na makatazo ya wanafunzi wajawazito kurudi shuleni yamesaidia kwa kias gani.

Amesema pamoja na matamko hayo pia Serikali imeweka mpango wa kupunguza changamoto kwa watoto wa kike ikiwemo kujenga mabweni na hosteli katika maeneo ambayo wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Mh. Ole Nasha ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi katika Halmashauri zao wanaendesha zoezi la ujenzi wa mabweni ili kuwaepusha wanafunzi hao kutembea umbali mrefu na lengo la kuwapeleka katika vyuo vya ufundi wanafunzi wanaobebeshwa ujauzito ili kuwasaidia kujiepusha na unyanyapaa ambao unaweza kujitokeza.

Aidha Mh. Ole Nasha ametoa wito kwa wazazi na walezi Nchini kushirikiana na Serikali katika kutokomeza matukio ya kubebeshwa mimba wanafunzi na inapotokea hivyo wahusika wafikishwe katika vyombo vya dola huku pia akitumia fursa hiyo kuwatakia mtihani mwema wanafunzi wote wa shule za msingi Nchini ambao leo wameanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi.

Mwaka 2017 Rais Dr. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Chalinze mkoani Pwani alitangaza chini ya utawala wake hakuna mwanafunzi majamzito atakaeruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo na mwanaume aliehusika kumbebesha mimba mwanafunzi atafungwa miaka 30 jela

No comments:

Post a comment