WAZIRI wa Madini Doto Biteko akizungumza na wananchi wa wilaya ya Tunduuru wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma
 MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Waziri wa Madini Doto Biteko
MKUU wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Julius Mtatiro akizungumza katikati ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kulia ni Waziri wa Madini Doto Biteko 


WAZIRI wa Madini Doto Biteko amewataka watu wanaotorosha madini hapa nchini kwenda nchi za nje waache mara moja biashara hiyo kwani ni zilipendwa badala yake wayapeleke kwenye masoko mbalimbali ili kuweza kuyauza.

Biteko aliyasema hayo akiwa kwenye ziara yake mkoani Ruvuma ambapo alisema kwamba badala yake wafanyabiashara hao kupeleka madini yao na wayauze huku akieleza iwapo wanataka kibali cha kusafirisha madini watapata ndani ya masoko hayo.

Alisema kwamba unaweza kununua madini ukafungiwa na unaweza kusafirisha huku akiwaomba viongozi wa serikali watu wa wizara ya madini, mamlaka nyengine wawasaidie watanzania kunufaika na madini yao.

 “Ndugu zangu tusiwafanye watanzania wawe watoshaji wa madini tukiwa tunawafuata kila wakati utawafanya watu wasifike kwenye soko na wafurahie kufanya vitendo ambavyo sio vizuri “Alisema.

Waziri Biteko pia aliwataka watanzania wajanja wajanja wanaotaka kuuza madini feki teknolojia imekuwa hivi sasa hivyo wasijiingize kwenye matatizo kwa maana hawatasalimika.

“Katika mkoa wa Ruvuma na nchi ya Tanzania kuna maeneo yanayozalisha madini ya vito kwa wingi ni Tunduru ipo na ni wilaya zinazozalisha vito kwa wingi.. Tulikuwa tunafanya baishara kubwa lakini maisha ya watu wa tunduru yalikuwa hayaonyeshi kama kulikuwa na maisha ya namna hiyo”Alisema

“Madini yalikuwa yanatoroshwa kupelekwa nje ya nchi lakini Rais wetu Dkt John Magufuli akasema tufunge breki tuanzisha masoko ya madini hatua ambayo imeweza kuwasaidia sana sekta ya madini hapa nchini “Alisema

Alisema kwamba katika kumbukumbu zake mwezi February  mwaka jana alikutana na wageni wengi ambao wananunua madini kupitia leseni za wenyeji huku wakiwapa kupewa fedha kiduchu jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza watanzania wengi.

Waziri huyo alisema kwamba lakini Rais Dkt Magufuli akawataka watengeneze utaratibu wa kusimamia madini hayo ili yaweze kuwa na manufaa kwa watu wa tunduru na mkoa kwa ujumla.

“Watu wa Tunduru wanahitaji fedha wajenge nyumba nzuri,fedha wasomeshe watoto,wale vizuri wakae kwenye mazingra mazuri hata mtu akiihtaji kuoa aweze kuona bila mkopo”Alisema



Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: