Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mwenyekiti wa Mtaa  wa Olasiti kati ,Bruno Mbole ameanza juhudi za kukarabati barabara ambazo zilikua hazipitiki katika mtaa wake hasa kipindi cha mvua kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kumwaga vifusi vya moram na kukarabati barabara hizo ili ziweze kupitika kwa kipindi chote.
Akizungumza mara baada ya Ziara ya Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi kutembelea barabara hiyo amesema kuwa kipindi cha mvua barabara hiyo haipitiki kutokana na maji kujaa njiani  hivyo wamejipanga kushirikiana na wadau kupata mabomba yatakayosaidia kuhamisha maji hayo ili yafate mkondo wake wa asili badala ya kupita barabarani.
“Tunashukuru tumeweza kupata vifusi ambavyo tumevimwaga kama unavyoona tunaamnini kuwa tutapunguza adha kwa wananchi wetu wanaotegemea barabara hiyo” Alisema Bruno
Afisa Tarafa ya Elerai Titho Cholobi amempongeza Mwenyekiti huyo kwa ubunifu aliofanya na kuhamasisha  uchangiaji wa vifusi vya moram jambo ambalo linalenga kutatua kero kwa wananchi.
Cholobi ameahidi kuchangia lori la moram ili barabara hiyo iweze kupitika kirahisi kwa kipindi chote cha jua na mvua ,kiangazi na masika.

Diwani wa kata ya Olasiti Alex Marti  amesema kuwa wanashirikiana bega kwa bega katika kuhakikisha kuwa barabara hiyo inapitika na kuwa msaada kwa wananchi .
Mwenyekiti wa CCM kata hiyo Amon Ndoto ameeleza kufurahishwa na jitihada zinazofanywa na Afisa Tarafa na Mwenyekiti wa Mtaa  wa Olasiti kati  katika kusimamia miradi ya serikali na kuitembelea kila mara ili iweze kuleta tija kwa wananchi kama ilivyotarajiwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: