NA SALVATORY NYANDU
Mwalimu wa Shule ya Msingi Namagubu wilayani ukerewe Mkoani Mwanza, Joseph Msafiri anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumjeruhi Mpenzi wake Neema Kabulu kwa kitu chenye ncha kali (panga) kwa wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea septemba 6 majira ya saa mbili usiku katika nyumba ya kulala wageni iliyopo eneo la Old Shinyanga, mjini shinyanga.

Amesema Joseph  akiwa katika maandalizi ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake Neema nyumbani kwao walilala katika nyumba hiyo wakitokea ukerewe jijini Mwanza lakini ilipofika usiku alimkata kwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni, tumboni na mkono wa kulia na Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

 Kamanda Abwao amesema Majeruhi anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya kutokana na kujeruhiwa katika tukio hilo na wanaendelea kumshikilia Joseph kwaajili ya upelelezi.

Amefafanua kuwa baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili ambapo eneo la tukio Jeshi la polisi wamepata   panga lililotumika kufanya tukio hilo, na Nguo zenye damu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: