Sunday, 8 September 2019

Dc Sabaya amtumia salamu Mbowe kuhusu ufalme wa Hai


Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amemtumia salamu Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA  Freeman Mbowe, kwamba muda wake wa kuendelea kuongoza katika jimbo la Hai umefika ukomo kwa sababu mambo yote waliyokuwa wanayapigia kelele yamekwishashughulikiwa.
Hayo ameyabainisha leo Septemba 8, katika kampeni ya Manyara ya kijani iliyozinduliwa mjini Babati na Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James, na kusema kuwa kipindi kilichopo sasa si cha kupiga kelele kama ilivyokuwa awali bali ni kipindi cha kumpa nafasi Rais kuendelea kufanya yaliyo mazuri zaidi.
''Mimi nimetumwa na Rais Magufuli kuwa DC wa Hai, lakini nimeteuliwa na M/kiti wa CCM, mambo ya kuwa neutro mnayajua ninyi wenyewe, mimi ni DC na ntawatangazia leo kwamba, kule Hai Ufalme umeshafitinika'' amesema DC Sabaya.
DC Sabaya ameongeza kuwa kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Tano ni cha tofauti kwani hata zile kelele za wizi kama vile ESCROW, IPTL zilizokuwa zinapigwa na wapinzani kwa sasa hazipo kwani amepatika Rais aliyethubutu kurudisha nidhamu ya Serikali.

No comments:

Post a comment