Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro  amekabidhi vifaa  muhimu  kwa shule ikiwemo mashine ya kuchapisha (printer)  kwa ajili ya mitihani na majiribio ya ndani ya shule lengo ikiwa ni kuboresha miundombinu ya elimu na kukuza kiwango cha elimu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo amewataka  Maafisa Tarafa ,waratibu wa elimu kata na wakuu wa shule kuhakikisha kuwa wanatumia vifaa hivyo katika kukuza ubora wa elimu na kuongeza ufaulu katika shule zao.
Gabriel amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira bora ya elimu ili kuhakikisha kuwa taaluma inakua kwa kiwango cha juu.
Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kazi nzuri  ya kukabidhi vifaa hivyo vitapunguza gharama za uchapishaji wa mitihani ya ndani
Share To:

msumbanews

Post A Comment: