Monday, 2 September 2019

Basi la Mwendokasi lateketea kwa moto katika Kituo Kikuu cha Kimara Dar

Basi la Mwendokasi lililokuwa linatokea Mjini kuelekea Kimara Mwisho limeteketea kwa moto eneo la Kimara Mwisho Dar usiku wa kuamkia leo lakini  hakuna madhara yaliyojitokeza kwa Binadamu, 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Teopista Malya amesema bado chanzo cha ajali hakijajulikana hadi pale uchunguzi utakapofanyika.

Amesema basi hilo lilitoka Mjini likiwa na abiria na lilipofika eneo la Kimara Mwisho walifanikiwa kushuka kabla halijateketea kwa moto.

No comments:

Post a comment