Sunday, 25 August 2019

PICHA : WANAWAKE ZAIDI YA ELFU 12 KILIMANJARO WAELEZWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM


Dhamira ya UWT Taifa chini ya Mwenyekiti Mama Gaudentia Kabaka ya kuwaelezea maelfu ya wanawake wa Tanzania utekelezaji wa Ilani ya CCM leo hii umeendelea kufanyika Moshi.

Maelfu ya wanawake wa Kilimanjaro wamepata kuelezewa utekelezaji wa Ilani katika mkoa wa Kilimanjaro na kuondoa dhana ya kuwa mkoa huo umetengwa na Rais Magufuli.
"Mhe. Mgeni rasmi dhamira ya UWT nikuwaeleza wanawake wa Tanzania utekelezali wa Ilani ya CCM kwani ndio wanufaika wakubwa na wapiga kura wa uhkika" alisema mama Kabaka.

Katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wa Serikali, Manaibu Mawaziri  walieleza  jinsi serikali ya awamu ya tano inavyogusa maisha ya watu wa Kilimanjaro.
"Serikali haijawacha kama wanavyo vumisha watu wengine miradi hii ya umwagiliaji zaidi ya 18% nchi nzima iko Kilimanjaro" alisema mwakilishi toka wizara ya Kilimo.

Akitoa hotuba yake Mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwa niaba ya Spika  Ndugu Jobu Ndugai aliyasoma mambo 15 yalifanywa na Rais Magufuli.
"Naomba niyasome mambo haya kwa niaba ya Spika ameandika ili wanawake wa Kilimanjaro muyafahamu" alisema Dkt. Tulia

1. Serikali imeleta nidhamu kwa watumishi wa umma.
2 Serikali inapambana  na vitendo vyote vya Rushwa katika taifa.
3. Kupambana na mafisadi hadi kupelekea kuanzisha mahakama.
4. Kupunguza natumizi yasiyo ya lazima kwa serikali safari za nje.
5. Kusimamia taratibu za makusanyo ya serikali na kuongeza pato la taifa.
6. Kuongeza kasi za ujenzi wa miundombinu.
7. Kuboresha shirika la ndege la taifa. ATCL
8. Kudhibiti utoroshwaji wa Madini.
9. Mpango wa kutoa elimu bila malipo.
10. Upatikanaji wa maji.
11. Kusikiliza migogro ya ardhi.
12. Kuhakiki mali za chama na serikali.
13. Kuhakikisha kilimo kinawanufaisha wakulima.
14. Kugawa vitambulisho kwa wafanya biashara wadogo.
15. Bajeti kugusa maisha nakupnguza kodi zenye kero jumla ya kodi 57 zimetolewa.

Maelefu ya wanawake na wananchi wa Kilimanjaro walipiga makofi na vigelegele  kupongeza utekelezaji mkuu wa mambo mengi wa serikali ya awamu ya Tano.

"Hakika tumepata vya kusema kwa majirani zetu yani kwanini CCM iendelee kushika hatamu" alisema Veronika Mshana mkazi wa Moshi.
UWT Imekamilisha kazi hapa Kilimanjaro na wananchi wameahidi kura za aksante kwa CCM kwa chaguzi zote zijazo.No comments:

Post a comment