Wednesday, 28 August 2019

MASHIRIKA YATOA ELIMU YA LISHE BORA KWENYE MBIO ZA MWENGE NZEGA TABORA


Mwananchi aliyefika kutembelea banda la mashirika mawili ya yasio ya kiserikali ya Save the Mother and Children of Central Tanzania (SMCCT) la mkoani Singida na Christian Education and Development Organization (CEDO) la mkoani Tabora, akielezea kufurahisha na elimu ya masuala ya lishe kwa mama mjamzito iliyotolewa na mashirika hayo kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Nzega mkoani Tabora jana . Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la CEDO, Japhet Kalegeya na katikati ni Mkurugenzi wa SMCCT, Eveline Lyimo. 


Maonyesho yakiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Nzega. 

MASHIRIKA Mawili yasio ya kiserikali ya Save the Mother and Children of Central Tanzania (SMCCT) la mkoani Singida na Christian Education and Development Organization (CEDO) la mkoani Tabora yametoa elimu kwa jamii kuhusu lishe bora kwa mtoto ikiwemo suala la elimu, afya na ulinzi wa mtoto Wakati wa monyesho ya viazi lishe katika hafla ya kuupokea Mwenge wa Uhuru Wilayani Nzega, Mkoani Tabora.

Maofisa wa taasisi hizo wakitoa  elimu kwa jamii juu ya haki ya mtoto kupata lishe bora katika maonyesho ya bidhaa zitokanazo na viazi lishe kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani hapa juzi  walisema mtoto anapaswa kupata lishe hiyo yenye virutubishi kama viazi lishe na kula vyakula vya aina mbalimbali tangu akiwa tumboni mwa mama yake.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Save Mother and Children Central of Tanzania (SMCCT ) Evaline Lyimo alisema lishe bora kwa ntoto uanzia tangu akiwa tumboni mwa mama yake.

" Lishe bora inasaidia kuboresha ukuaji wa mtoto kimwili na kiakli,  kupungua uwezekano wa kupata mtoto mwenye uzito pungufu na kupunguza udumavu"

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CEDO, Japhet Kalegeya alisema vyakula vya aina mbalimbali na vyenye virutubisho vinahitajika sana katika ukuaji wa mtoto na ndio maana huwa wanamsisitiza mama mjamzito kuvitumia na kupata muda wa kupumzika.

"Tumekuwa tukisisitiza sana matumizi ya vyakula hivyo kwa mama mjamzito jambo linalosaidia mtoto akizaliwa kuwa na afya njema na kumuepusha na utapiamlo na ugonjwa wa manjano" alisema

No comments:

Post a Comment