Na Lucas Myovela_Arusha.
Afisa wa Jeshi la Polisi akiwaeleza viongozi wa Halmashauri hiyo kutoka nje ya Ukumbi kama alivyo pewa Amri na Dc Jerry Muro.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndg Jerry Muro amelazimika kuamuaru jeshi la polisi kuwatawanya madiwani na washiriki waliyokuwa ndani ya ukumbu wa mikutano wa Halmashauri hiyo kwania ya kuepusha vurugu zilizo anzishwa na madiwani wa halmashauri hiyo.

Awali myenyekiti wa baraza hilo la madiwani Ndg Wille Njau alisoma ajenda ya kikao hicho na kutoa muongozo kwa madiwani wengine ili kuchangia ajenda hizo na kuruhusu maoni na mapendekezo ya madiwani hao.

Vurugu hizo zilianza ambapo diwani wa kata ya Kikwe Ndg Paul Samweli shango (CCM)  aliomba muongozo wa kutaka kujua juu ya kuhudhuria kwa diwani wa kata ya Maluvango Bi Digna John Nassari ilihali mwenyeketi wa halmashuri hiyo alitangaza kuwa diwani huyo siyo diwani tena kupitia chadema na amevuliwa uwanachama wake.

Katika mvutano huo uliyomuhusisha diwani wa kata ya Maluvango (chadema) kwa 100%,juu ya maudhulio yake ya kikao hicho pasipo taarifa ambapo alitolewa kwa utaratibu na kanuni zao mnamo tarehe 18 May mwaka huu na leo hii ameudhulia kikao pasipo utaratibu na sheria zao na kanuni kitu walicho hoji kama baraza hilo nila mtu mmoja au wawili.

"Mh mwenyekekiti hatuwezi kuendelea na baraza kwasasa mpaka utakapo tuambia kwanini Mh Digna ameudhulia kikao pasipo utaratibu wala kutueleza madiwani wenzake na ulimuondoa mwenyewe kwa utaratibu na ukatangaza kwamba amevuliwa uananchama wa chama chenu leo hii hautaki kutueleza kwahili halivumiliki hata aje nani hapa hakuna kikao mpaka utakapo weka wazi" walisema madiwani hao.

Takribani dakika 100 za mabishano kati ya madiwani na mwenyekiti wa  Halmashauri ya Meru hazikuweza kuzaa matunda ya maelewano na kuchukua sura mpya baina ya madiwani wa ccm kusimama kupinga uendeshwaji mbuvu na wakiholela kwa baraza hilo na kuungwa mkono na madiwani wa chadema ambao pia hawana imani na mwenyekiti wao licha kutokana na chama chao.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro,Akitoa tamko la kuhairisha kikao cho cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Meru baada ya mvutano wa muda mrefu.

Mara baada ya mvutano mrefu ndipo busara za Dc Murro zikafuata za kuamuru kuhairishwa kwa baraza hilo hadi pale watakapo kaachini na kuelewana na kumtaka mwenyekiyi huyo awe na busara ya kiuongozi maana wote wanawawakilisha wananchi waliyo wachagua na kumtaka ajitathimi juu ya mwenendo wake wa uongozi kama mwenyekiti wa Baraza.

"Mwenyekiti toka nimekaa hapa hakuna hoja yeyeote iliyosikilizwa zaidi ya marumbanao na madiwani wako wote kusimama kwa nia ya kutokuwa na imani na wewe na wewe hutaki kuwaweka sawa ili muelewane sasa nilihairisha baraza hili kwa maana naona amani imesha vurugika na kama mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru kuanzia sasa watu wote mtoke nje nimelihalisha baraza msije pigana mbele yangu kama mnamambo yenu huko huko nje siyo hapa hapa tumekuja kutatua kero za wananchi". Alisema Dc muro.

MTITI WA NJE YA BARAZA BAADA YA DC KUCHOMOA BETRI.

Kwa upande wake diwani aliyevuliwa uanachama anaeleza kwamba Mwenekiti wa baraza hilo alisha andikiwa barua na katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Bw Vicent Mashinji mnamo tarehe 28 May 2019 na kwaelekeza viongozi wa chadema kumrudishia unachama wake diwani huyo pamoja na cheo chake mara moja kwa kile alicho andika kuwa hawakuzingatia kwa kutokufuata utaratibu.

"Nilitolewa ndani ya baraza tarehe 18 May 2019 nikatoka salama na tarehe 25 May mwaka huu nikakata rufaa ili kupinga kuvuliwa uanachama wangu pasipo kujua kosa halali ni lipi na kwa bahati nzuri tarehe 28 nikajibiwa na katibu mkuu wa chadema lakini sasa cha kushangaza mwenyekiti wetu wa baraza hataki kuwatangazia madiwani wenzangu kwamba nimeshinda na nimerudi katika nafasi yangu hii siyo haki maana siku ananitoa nje nilidhalilika sana lakini nilikubali na kumtanguliza mungu wangu mbele kwanini leo hataki kukiri mbele ya Baraza hili kuwa mimi ni diwani halali na wanilipe stahiki zangu zote walizo zizuia hapo awali za toka mwezi wa nne mwaka huu". Alisema Digna Nassari.

Ikumbukwe tu baraza hilo kwasasa linaingia katika sura mpya baada ya madiwani waliyo kuwa wa chadema na kuhamia chama cha mapinduzi ccm kwa kile kilichodaiwa ni kumuunga mkono Rais Johm Magufuli katika utendaji wake makini na madiwani hao kuwa na nguvu kibwa ya kutetea wananchi wao waliyo wachagua.

Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: