Sunday, 18 August 2019

Kiswahili Chapitishwa Kuwa Lugha Rasmi ya SADC

Rais Magufuli amesema Wakuu wa Nchi wa SADC kupitisha lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya 4 itakayotumika katika shughuli rasmi za Jumuiya hiyo,ni heshima kubwa kwa Mwl Nyerere ambaye aliongoza Nchi nyingi Afrika katika  Mapambano ya kudai Uhuru akitumia Kiswahili.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 18, 2019 katika kilele cha  mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi, Rais Magufuli amesema katika kikao kilichofanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakuu hao kwa pamoja wamekubaliana lugha hiyo ianze kutumika.

Lugha zilizokuwa zikitumika katika nchi hizo 16 ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa.  Kuanzia sasa Kiswahili kitatumika katika mikutano ya jumuiya hiyo pamoja na machapisho yake mbalimbali.

No comments:

Post a Comment