Friday, 9 August 2019

ELIMU INAHITAJIKA KWENDA NA MIPANGO YA SERIKALI-DKT AKWILAPO


katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akifungua Mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu kujadili Usimamizi wa Mafunzo ya Ualimu iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Mafunzo ya Elimu Agusta Lupokela akitoa maelezo katika mkutano wa kujadili sekta ya Elimu kwa Ualimu.
Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu Ignas Chonya akizungumza na waandishi kuhusiana na mafanikio ya mradi huo.


Mwenyekiti wa Walimiki wa Vyuo vya Ualimu Binafsi Mahamood Mulingo akizungumza namna ya uendeshaji wa elimu kutokana na mahitaji yaliyopo kwa muda uliopo.
Sehemu ya wadau katika mkutano huo.
picha ya pamoja wakuu wa Vyuo vya elimu katika picha ya pamoja


Serikali imesema kuwa katika kwenda na mipango na mikakati mbalimbali kunahitaji kuangalia sekta ya elimu kwa ajili ya kuzalisha wataalam wa kufundisha wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo wakati akifungua mkutano wa Elimu ya Ualimu katika kujadili Usimamizi wa Mafunzo ya Ualimu uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mkutano huo ni kuangalia mambo mbalimbali ya kuandaa Walimu pamoja na kuangalia mitaala inayokwenda na wakati.Dkt. Akwilapo amesema kuwa serikali inakwenda na mipango mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu inayoendana na mwelekeo ya mipango hiyo.

Amesema kuwa katika mkutano watajadili na mitaala namna ya kuboresha kwenda na mazingira yaliyopo na mabadiliko ya mitaala ni kutokana na serikali inavyotaka katika uboreshaji wa elimu nchini.

Aidha amesema watalaam waliokuwepo katika mkutano huo ni wabobezi katika mafunzo ya Vyuo vya ualimu ambao wanaweza kushauri serikali katika kuandaa Walimu wataokwenda kufundisha wanafunzi wa Msingi na Sekondari.

Nae Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Mafunzo ya Elimu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Agustina Lupokela amesema mkakati wa malengo ya Seksheni kwa mwaka 2019/2020 inayoongozwa na Kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa la Uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia uchumi wa Viwanda.

Amesema mikakati yote imejikita katika kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa walimu wa masomo ya Sayansi,Hisabati na fani za Ufundi ili kufanikisha azima ya serikali.

Mratibu wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Ignas Chonya amesema kuwa Mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania na Japan na unaendelea kufanya vizuri katika sekta ya Elimu.

Amesema kuwa mradi huo umeanza hadi sasa mwaka wa tatu na matokeo yake katika uboreshaji wa Shule pamoja na rasiliamali watu kuongezewa ujuzi.