Pichani: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Themi wakiwa na kiti na meza walivyo patiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.
Pichani: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Olmoti wakiwa na kiti na meza walivyo patiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.
Pichani: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sombetini wakiwa na kiti na meza walivyo patiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt.Maulid Suleimani Madeni amekabidhi madawati 936 yenye thamani ya shilingi 79,227,850 katika shule za msingi zilizopo Halmashauri ya jijini Arusha.  

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Valentine Makuka ametaja shule hizo ambazo ni Sekondari ya Baraa madawati 120, Olmoti 185, Sombetini 270, Themi 150 na Naura 211 lengo likiwa ni kuboresha elimu kama ilivyo kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano.
Mwalimu Makuka amesema kwamba utengenezaji wa madawati haya umekuwa ni wa gharama nafuu baada ya kutumia karakana ya Shule ya msingi na Ufundi Kaloleni ambapo awali wazabuni ndio waliokuwa wakitumika kutengeneza madawati ambayo ilikuwa inagharimu fedha nyingi.
“Kwa kutumia karakana ya shule ya msingi na ufundi Kaloleni kiti na meza moja hadi kufikishwa shuleni imegharimu shilingi 96,000 kulinganisha na mzabuni ambapo inagharimu shiling 150,000” alisema Mwalimu Makuka.
Pamoja na lengo la kupunguza gharama Mwalimu Makuka alisema kuwa kutengeneza madawati katika Karakana hiyo ni fursa ya kuiwezesha kujiendesha kiuchumi.
Naye Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi na Ufundi Kaloleni  Bi. Nemhina Mfikilwa  amemshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni kwa kuipa kipaumbele Karakana iliyopo katika shule yake kwani ameonesha uzalendo na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kubana matumizi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: