Afisa mwandikishaji Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmannuel Mkongo akizungumza na mwandishi wetu,amesema mwitikio wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura jimbo humo upo vizuri  kwani Katika Kata alizotembelea Akheri,Kwarisambu, Poli wananchi wanajitokeza kwa wingi haswa vijana waliotimiza miaka 18 wanaojiandikisha kwa mara ya kwanza, pia katika Kata hizo mwitikio ni mkubwa zaidi maeneo yenye mikusanyiko ya watu unaotokana na shughuli za kibiashara tofauti na maeneo ya pembezoni ambapo mwitikio ni mdogo.
Mkongo amesema hakuna changamoto iliyojitokeza ikaahiri zoezi  hilo hadi sasa kwani baadhi ya Mashine za Bvr  zilizo kuwa na itilafu na shindwa kuchapa  vitambulisho ilitatuliwa na wataalamu wa TEHAMA  "Nilipopita kukagua zoezi hili la uandikishaji  Kituo cha Kupigia chuo cha Mifugo Tengeru LITA  nilikuta BVR KIT haifanyi kazi  na kwa sasa wataalam wa TEHAMA mameshatatua na wananchi wanapata huduma"ameeleza Mkongo.
Mkongo ametoa rai kwa  Wananchi kuhifadhi vizuri vitambulisho vyao vya  Mpiga Kura  kwani wengi wao wanaokwenda kuboresha taarifa zao  imeoneka vitambulisho vyao vya awali kuharibika (vunjika) kutokana na kuvikali vikiwa mifukoni nk, "Ndugu Mwananchi Kitambulisho cha mpiga kura ni kitambulisho muhimu kwani kinakupa haki ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Rais ,Mbunge na Diwani hivyo hamna budi kuvihifadhi vizuri" amesisitiza Mkongo. 
Mkongo ametoa rai kwa wananchi ambao wanataka kurekebisha na  kuhamisha taarifa zao,kufuta taarifa zao, wanaotimiza umri wa  miaka 18 ifikapo tarehe 28 Mwezi Octoba 2019 na wenye miaka umri wa 18 ambao hawajajiandikisha kujitokeza na kujiandikisha na kupata vitambulisho vya Mpiga Kura kwani zoezi hilo litadumu kwa siku saba tu, kuanzia tarehe 18 /07/2019 hadi tarehe 24/07/2019.
PICHA ZA TUKIO
Afisa uandikishaji jimbo la Arumeru Mashariki ,ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru NDG.Emmanuel Mkongo akifuatlia utendaji wa BVR KIT Operator Ndg.Mbora Kweka ,katika kituo cha kupiga kura Mkwakirika Kata ya Poli.
Ndg.Ayob Mbise akiwa ameripoti kituo cha kupiga kura Nkwakirika kwaajili ya kujiandikisha.

Mwandishi msaidizi Ndg.Christopher Saimon akimwelewesha mama aliyefika kujiandikisha ,BVR KIT operator akimwandikisha Ndg.Ayoub Mbise.
Ndg.Ayob Mbise akitia saini yake kwenye Mashine ya BVR
Ndugu Ayob Mbise akiweka alama za vidole wakati wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura.
Ndg.Ayob mbise akiweka alama za vidole wakati wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura.
Zoezi la kujiandikisha likiendelea katika Kituo cha kupiga kura Poli chama cha Msingi.
Wananchi wakipata ufafanuzi katika kituo cha  kupiga kura Poli chama cha Msingi.
Afisa uandikishaji Jimbo la Arumeru Mashariki akipokea maelezo toka kwa BVR KIT operature Geturd Mkumbwa na Mwandishi msaidizi Nakaji Lukumay kituo cha kupiga kura Polli chama cha Msingi.
Afisa uandikishaji Jimbo la Arumeru Mashariki akikagua utendaji wa BVR KIT operato Ndg.David Josiah, kituo cha kupiga kura Makumira Consumer.
Zoezi la uandikishaji daftari la kudumu la mpiga kura likiendelea katika kituo cha kupigia kura Makumira Consumer.
BVR KIT , kituo cha kupiga kura Makumira Consumer, Ndg. David Josiah akimkabidhi  kitambulisho cha mpiga kura miongoni mwa wananchi waliojitokeza kuboresha taarifa zao katika daftari la mpiga kura.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: