MKUU wa Mkoa wa Katavi ,Juma Zuberi Homera  ameipongeza Halmashauri ya Mpimbwe kwa mwenenendo mzuri wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya kwa kufikia 87% na hivyo kuonekana kuendana na kasi nzuri ambayo itasaidia kumalizika kwa wakati na hatimaye kuanza kutumika

Pongezi hizo zinatokana na  kasi kubwa ya ujenzi wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Erasto Siwale ambaye amekuwa akisimamia kwa umahiri mkubwa miradi na kuwaunganisha watumishi kuwa kitu kimoja.

Hospitali hii inajengwa kwa sh.Ts Bilion 1.5 ambapo pia amewapongeza pia wafanyakazi na mafundi wanaoijenga hospitali hiyo na kuwataka waendelee kuwa wazalendo na kutotumia saruji na vifaa vingine kinyume na matakwa ya serikali.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaeleza wananchi waliokuwa hospitalini hapo kuwa ujenzi wa Hospitali hizo za mkoa mzima wa Katavi ni Jitihada za serikali ya CCM ya awamu ya Tano katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015-2020 ibara ya 49,50 inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikisimamiwa vyema na waziri wa Nchi Ofisi Ya Rais Tamisemi Mhe Suleiman Jafo.

Aidha pia amewataka wananchi na mafundi kuhakikisha Hospitali inakamilika kwa wakati ili waendelelee kufurahia matunda yanayotokana na serikali ya awamu ya tano ambayo imejipambanua katika kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto ambazo zinawakabili wananchi ikiwemo za Afya

Hata hivyo RC huyo amewahakikishia wananchi wa Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi ujenzi wa barabara kiwango cha lami wenye urefu wa KM 1.7-Mpaka 2  kwa Bajeti ya mwaka 2019/2020 Katika Mji wa Uservya chini ya wakala wa Barabara Tanzania ,Tanroad.

Aliongeza kwamba pia hayo yatafanyika sambamba na uanzishwaji wa Benki mojawapo katika mji huo ambao una uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara na chakula pamoja na Kata ya majimoto mkoani Katavi.
Share To:

Post A Comment: