Thursday, 11 July 2019

HALMASHAURI YA ILALA KUWAANDALIA TUZO SOS CHILDRENS VILLAGES

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Kumbilamoto akizungumza katika  mafunzo  ya majadiliano  na wadau mbalimbali juu ya uwajibikaji wa jamii na Watendaji wa Serikali katika suala la ulinzi na Usalama wa Mtoto kata ya Chanika na Zingiziwa Manispaa ya Ilala leo,mafunzo ya siku tatu yameandaliwa na shirika la SOS Childens Villages(kulia)Mwenyekiti wa Mtaa Sefu Mwera na Ofisa Mtendaji wa Kata Chanika Deodatus Likonga   (PICHA NA HERI SHAABAN)
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Kumbilamoto akipokea maandamano katika  mafunzo  ya majadiliano  na wadau mbalimbali juu ya uwajibikaji wa jamii na Watendaji wa Serikali katika suala la ulinzi na Usalama wa Mtoto kata ya Chanika na Zingiziwa Manispaa ya Ilala leo,mafunzo ya siku tatu yameandaliwa na shirika la SOS Childens Villages   (kushoto )Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo(PICHA NA HERI SHAABAN)
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala omary Kumbilamoto akisalimiana na viongozi wa Shirika lisilo la kiserikali la SOS childens villages (katikati)Diwani wa viti maalum Manispaa ya Ilala neema Nyangarilo
 Naibu Meya wa manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akisalimiana na Mwenyekiti wa kikundi cha Sayari Nipael Joshua Picha na Heri Shaaban
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akiwa katika picha ya pamoja na wadau kwenye mafunzo ya Sos childres Villages(kushoto)Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo na Mwenyekiti wa Sayari Nipael Joshua(Picha na Heri Shaaban)

Na Heri Shaaban

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imesema itaanda tuzo maalum kwa kutambua mchango wa taasisi ya kijamii ya Shirika la SOS Childrens Villages iliyopo manispaa ya Ilala kutokana na shirika hilo kujikita zaidi kuhudumia jamii.

Hayo yalisemwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto wakati wa Ufunguzi wa mafunzo ya wadau mbalimbali juu ya uwajibikaji wa jamii na Watendaji wa serikali katika suala ulinzi na Usalama wa mtoto katika kata za Chanika na Zingiziwa.

"Halmashauri ya Ilala tunatambua mchango wenu katika jamii ambao mnatoa katika kata za Chanika na Zingiziwa na manispaa ya Ilala kwa ujumla tunaandaa utaratibu wa kuwatafutia tuzo kutambua mchango wenu nitazungumza na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala katika ili nawaomba muendelee katika utoaji wa elimu na kuisaidia jamii"alisema Kumbilamoto

Aliwataka watekeleze majukumu yao ya shirika hilo pindi watakapoitaji msaada serikali itawasikiliza kupitia halmashauri ya Ilala .

Kwa upande wake Ofisa Mradi wa kuimalisha Familia Godwin Mziray alisema shirika la Sos Childrens Villages Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali limejikita katika kuhudumia watoto yatima na Walio katika mazingira hatarishi hatari ya kupoteza kupoteza malezi.

Mzirai alisema shirika hilo linatekeza miradi mitatu Kuimalisha familia ,mradi wa kuimalisha familia ambao ulianza mwaka 2013 mradi una hudumia kaya 132 zenye watoto 500 waliopo katika mazingira hatarishi.

Aidha alisema mradi mwingine wa kucheza na kujifunza ulianza mwaka 2016 una lenga kuboresha mazingira ya kujisomea na kufundishia ili watoto waweze kupata elimu bora.

Alisema dhumuni kuu la shirika hilo linashughulikia mambo makuu mawili hasa ndio msingi wa utendaji na utekelezaji wa shughuli za shirika,malezi na ulinzi wa usalama wa watoto katika kata za Chanika na Zingiziwa Halmashauri ya Ilala maeneo ambayo watoto wapo katika hatari kubwa kutokana na vitendo vya kikatili vinavyotokea na vinavyofanywa kuanzia ngazi ya familia hasa watoto wenyewe kwa wenyewe.

Akizungumzia changamoto alisema tatizo kubwa lililpo ni uwajibikaji wa jamii na viongozi wenye dhamana bado ipo chini linaitaji jicho la ukaribu na elimu kuhusiana na maswala ya uwajibikaji wa jamii kwenye kutekeleza majukumu yao na kuwafanya watumishi wa serikali wawajibike.

Pia waliomba kufufuliwa kwa mchakato wa uundwaji wa sheria ndogondogo kama lilivyoanza ngazi ya kata ili upate baraka .

Mwisho

No comments:

Post a comment