Tuesday, 9 July 2019

DC MJEMA HATOA AGIZO WATENDAJI WA YA ILALA WASIYUMBISHWE NA WANA SIASANA HERI SHAABAN

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ametoa agizo kwa Watendaji wa Halmashauri ya Ilala akiwataka Wafanye kazi wasiyumbishwe na Wana siasa.

Mjema alitoa agizo hilo Arnatogluo Manispaa ya Ilala leo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma ambapo manispaa hiyo waliazimisha kwa kuongea na watendaji,Wakuu wa Idara na Watumishi.

"Nawaomba  punguzeni   urasimu katika utekelezaji wa miradi ya serikali isiwe kikwazo katika utekelezaji wa miradi,iwe choo,barabara,shule,pia mtendaji lazima ujue huo mradi ,na uweze kusimamia" alisema Mjema.

Alisema kila  kiongozi aliyopo Manispaa hiyo mradi wowote lazima ajilizishe na kuuona asisimamie miradi hewa kwa kupewa makaratasi.

Aidha aliwapongeza katika utoaji huduma bora kwa wananchi, aliwataka kila mmoja kutekeleza malengo ya serikali ya awamu ya tano kwa weledi katika uwajibikaji .

Aliwataka kila wakuu wa Idara kutenga muda siku mmoja ya kila mwezi kusikiliza kero za watumishi wao, kwani wao ni muhimu katika Watanzania milioni 50  wao wamechaguliwa katika kuisaidia serikali watumie cheo chao vizuri bila kuyumbishwa kwa utekelezaji maagizo ya serikali kwa kuiwakilisha Ilala.

"Wilaya ya Ilala ulikuja kwa makaratasi yako kuomba kazi,hukuja na mwana siasa  hakuna mtu wa kukukwamisha tenda kazi kwa mujibu wa sheria"alisema

Aliwataka kuboresha idara ya afya kwa baadhi ya watumishi pamoja na upande wa mgambo   watolewe wote waletwe wengine .

Aliwataka wafanye kazi vizuri bila kutumia rushwa, Watendaji wote wawe wazalendo,wafanye kazi vizuri wasichafuliwe na virushwa vidogo vidogo ,wakastaafu vibaya.

Akizungumzia suala la ulinzi na usalama amewataka watendaji kuwa makini katika suala la uraia  na kuilinda amani yetu ,pia marufuku kuruhusu ngono zembe sehemu ya kazi kwani mtumishi wa umma ni ngao ya serikali.

Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano ya chama cha mapinduzi ndio mwajili wako wamekupa kazi hivyo lazima uwipe kipaumbele ,katika utekelezaji wa majukumu kwa kuitumia nafasi vizuri na kuwataka  waongeze kasi ya ukusanyaji mapato na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa maslahi ya Taifa hususani sekta ya viwanda sambamba na kuimalisha huduma za jamii.

Pia aliwapongeza kufanya vizuri idara elimu Msingi katika ufaulu na kuitangaza Ilala ,idara ya afya pamoja na Idara ya maendeleo kwa kufanya vizuri katika mikopo ya serikali ya Wanawake ,vijana na Watu Wenye Ulemavu.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri aliwataka Watendaji wake na Watumishi kutumia hotuba hiyo katika kujifunza na kufanya kazi kwa bidii .

Mwisho
Julai 8/7/2019
Ukumbi wa mikutano Arnatogluo
Manispaa ya Ilala

No comments:

Post a comment