Saturday, 18 May 2019

Wizara ya Afya washirikiana na TAMISEMI kuboresha huduma katika Sekta ya Afya


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Taasisi isiyo ya kiserikali( Path) inaendelea na vikao vyenye lengo la kuandaa mpango (blue print) utaoelezea namna gani mifumo itasaidia kuboresha huduma katika Sekta ya Afya nchini.

Katika kikao hicho jumla ya kamati ndogo ndogo sita ziliundwa lengo ni kuhorodhesha Wadau muhimu katika kila kamati hizo wataosaidia katika kutatua changamoto katika maeneo ya Sekta ya Afya.

Pamoja na hayo, kamati hizo zimejadili juu changamoto zinazoikumba Sekta ya Afya katika kila kamati zilizoundwa na namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufikia malengo ya kutoa huduma za Afya zilizo bora kwa kila Mtanzania.

Wizara ya Afya, TAMISEMI na Path inatekeleza mradi wa "Matumizi ya takwimu za Afya (Data Use Partnership)" chini ya ufadhili wa Taasisi ya Bill and Melinda Gate Foundation ili kuboresha huduma za Afya nchini.No comments:

Post a Comment