Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. George Kakunda katikati akimsikiliza Mmiliki wa kiwanda cha Hans Paul Satbiri Hanspaul wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho gambo
Waziri wa Viwanda na Biashara George Kakunda leo ametembela kiwanda cha Hanspaul kinachotengeneza magariya kusafirisha watalii kilichopo eneo la Njiro Jijini Arusha nakutoa maelekezo kwa taasisi za BRELA na tume ya Ushindaniwa kibiashara (FCC) kuangalia namna ya kampuni mbili za Hanspaul na RSA ya Moshi zinazotengeneza magari ya utalii zinaweza kufanya biashara zao kwa ushindani na kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Mhe Waziri ameyasema hayo ikiwa ni siku moja baada yakutembelea kiwanda cha RSA na kupokea malalamiko tokakwa wamiliki wa kiwanda hicho juu ya kuigwa kwa nemboyao ya kibiashara.
“…ninaagiza BRELA na FCC waje hapa sio kwa lengo la kufunga kiwanda hiki ila ni kwaajili ya kuhakikisha kwambautaratibu unawekwa vizuri ili uzalishaji wa Moshi uendelee naUzalishaji wa Arusha uendelee na hiyo ndiyo kauli yangu yamwisho kwani kiwanda hiki kimefanya uwekezaji mkubwa nawa kisasa na tumeshuhudia ubunifu mkubwa ikiwemoutenegenezaji wa magari yanayotumia umeme” alisema Mhe. Waziri.

Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul Satbir Hanspaulamemshukuru waziri wa viwanda na biashara kwa kutembeleakiwanda chao na kujionea uzalishaji.

“Sisi kama wawekezaji wazawa tunajivunia sana kuwa naserikali inayojali changamoto za wawekezaji, Tanzania badokuna fursa kubwa sana ya uwekezaji na sisi tumeamuakuwekeza nyumbani ndio maana pamoja na kiwanda hiki cha kutengeneza magari ya watalii tumefungua na kiwandakingine cha kutengeneza mifuko ya karatasi ili kutoasuluhisho baada ya serikali kupiga marufuku mifuko yaplastiki” alisema Satbir.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema waokama Serikali ya Mkoa wamejipanga kutoa ushirikiano kwawawekezaji wote walioko mkoani Arusha.

“Sisi kama Mkoa tunajivunia sana uwekezaji huu na kuwepokwa kiwanda hiki Mkoani Arusha kwani ni sifa kwa mkoawetu na nchi kwa ujumla, hivyo nipende kuwatia moyowawekezaji hawa wakati wowote wanapokumbana nachangamoto za kibiashara lengo letu ni kulinda brand zetu zandani” alisema Gambo.

Katika ziara yake Mhe Waziri pia ametembelea kiwanda cha Hanspaul Industries Limited kinachotengeneza mifuko yakaratasi kujionea uwekezaji mkubwa ambapo amewapongezawawekeaji hao kwa kuweza kutafuta suluhisho baada yakatazo la mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 01 June 2019.
Share To:

Post A Comment: