Friday, 10 May 2019

Watu 15 Wanusurika kifo baada ya Magari kugongana uso kwa usoNa. John Walter-Manyara

Watu 15 wamenusurika kufa baada ya gari aina ya Land Cruser yenye namba za usajili T 692 AVB iliyokuwa imebeba abiria 11 kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya VIX namba zake ni T 460 DED iliyokuwa na watu wanne.

Ajali hiyo imetokea leo Mei 10, Majira ya saa 1:57 asubuhi katika eneo la Sigino darajani Mjini Babati Mkoa wa Manyara baada ya gari ndogo lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye jina lake halijafahamika mara moja kupasuka gurudumu la mbele na kuhama njia na kukutana na gari hiyo ya abiria iliyokuwa ikiendeshwa na Peter Paulo ikitokea Babati Mjini kuelekea Haydom-Mbulu ,ndipo katika jitihada za kukwepa gari hiyo alizidiwa nguvu na kupinduka.

Kwa mujibu wa Dereva huyo "ajali hiyo imetokea wakati natokea babati naona jamaa anahama kabisa njia,nilijitahidi kumkwepa lakini kwa sababu pembeni kulikuwa na korongo,ghafla niksikia tu kishindo na sijajua kilichoendelea" alisema dereva huyo.

Kwa upande wa mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa magari yote yalikuwa katika mwendo wa kawaida.

Daktari aliyewahudumia majeruhi hao,  Dr. Mandala Adamu akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu amesema majeruhi 12 wamepokelewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara na hali zao zinaendelea kuimarika.

Askari wa usalama barabarani Mkoa wa Manyara walifika eneo la tukio.

No comments:

Post a comment