29A
Mkuu  wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza moja ya mwenyekiti  kwa uhamuzi aliochukuwa wa kuhamia ccm
32A
Mkuu wa wilaya akifungua rasmi ofisi ya kijiji iliojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya songoro.
11A
Katibu Tawala  wa wilaya ya Arumeru  mwalimu Jemsi Mchembe akiongea na wananchi wakati wa usinduzi wa ofisi hiyo ya kijiji 
…………………..
Na Woinde  Shizza ,Arusha
Wananchi wa metakiwa kujijengea tabia ya kufanya shuhghuli za  maendeleo   katika  vijiji vyao na sio kutegemea serikali kuwafanyia kila kitu .
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati akizindua ofisi ya kijiji cha  Nsongoro kilichopo  Wilayani Arumeru mkoani hapa ,ofisi iliojengwa kwa nguvu za wananchi.
Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiacha kufanya maendeleo katika vijiji vyao  kwa kudai kuwa  serikali ndio inatakiwa kufanya au kuwaletea  maendeleo katika vijiji vyao  kitu ambacho sio cha kweli .
“napenda kutumia wakati huu kuwapon geza sana wanakijiji  wa kijiji cha Nsongoro kwa hatua mliofikia ya kuuza miti ya kijiji pamoja na kujichangisha  na kujenga ofisi hii ya kijiji ambayo kwa miaka yote tang mwaka 1976  mlikuwa hamna ofisi ya kijiji  na mlikuwa mnatumia ofisi ya chama cha mapinduzi , unajua wananchi wengi wanafikiriaga maendeleo kama haya yanaletwaga na serikali tu kitu ambacho sio chakweli kwani wananchi pia mnaweza kufanya wenyewe  vitu kama hivi”alisema Muro
Kwa upande wake katibu tawala  wa wilaya ya Arumeru  mwalimu Jemsi Mchembe aliwapongeza wananchi hao na kuwaambia maendeleo ya kweli yanaletwa na watu wenyewe hivyo ni vyema kila mwananchi kujituma ili kuleta maendeleo katika nchi yake na sio kutegemea tu serikali iwaletee maendeleo .
Aidha aliwaambia maendeleo pia hayana chama  hivyo ni vyema wananchi kushirikiana bila kujali chama wala kabili kufanya vitu ambavyo vitawanufaisha wananchi kwa  ujumla na sio wananchi wale waliopo kipini hiki pia itawasadia ata wajukuu na vitukuu watakao kuja baadae.
Naye mwenyekiti wa kijiji  Cha Nsongoro alisema kuwa ofisi hiyo  ya kijiji imejegwa kwa nguvu za wananchi kwa ambao walikaa na kukubaliana kuuza miti ya  iliopo katikashamba la kiijiji ambapo walipouza walipata jumla ya shilingi  milioni 19  na katika fedha hizo shilingi milioni 17 zilitumika kujenga ofisi hiyo  ya kijiji na shilingi milioni 2 ilitumika kwa ajili kuvuna miti ilioyokuwa shambani
Wakai huo huo  Baada ya kumtuhumu Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro kuamuru
kushushwa kwa bendera za chadema ,  Wenyeviti wa vijiji vitano na
vitongoji viwili wa kata ya Songoro wameamua kukihama chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) nakujiunga  na chama cha mapinduzi (CCM)   kwa lengo la kumuunga mkono mkuu wa wilaya ya Arumeru katika harakati zake za kuleta maendeleo.
Wenyeviti ambao  Walirudi CCM ni pamoja na  Eliah Mathayo Mbise aliekuwa  mwenyekiti wa kijiji cha Songoro,Pokeali latiaeli Nnko wa kijiji cha mulala,  Sadikiel Solomon Ayo wa
kijiji cha Sura pamoja na  Elifasi sunguroi Nassari wa kijiji cha Kilinga.
Pia wamo wenyeviti wawili wa vitongoji  Anathe Eliah mbise kitongoji cha
meto kijiji cha mulala, pamoja na Sinyaeli ndetaulo mbise wa kitongoji cha kiuta
kijiji cha songoro mbali na hao pia aliekuwa katibu Mwenezi wa Chadema  kata ya Songoro 
George peter  Pallangyo pamoja na mwenyekiti wa Bawacha Bi Ekael felix wamelitangaza rasmi kurudi  chama cha mapinduzi hivyo  Kwa sasa kata ya Songoro vijiji vyake  vyote sita vimerejea chama cha mapinduzi.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea katibu wa CCM wilayani Arumeru Shabani Mdoe alisema kuwa  wamefanya uhamuzi mzuri kwani wameamua kuja kuung amkoano juhudi  za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: