Monday, 6 May 2019

Wamiliki wa vyombo vya habari watakiwa kumuenzi Dkt. Mengi
Chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari Nchini(MOAT), kimetoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya Habari Nchini kutumia vyombo vyao kumuenzi aliyekuwa Mtendaji wa Makuampuni ya IPP, Dkt. Reginald A. Mengi.

Akizungumza leo Mei 5, 2019, katibu mtendaji wa MOAT, Henry Mwinika amesema hayo akiwa katika kikao maalum walichofanya na waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya Habari na kuwaomba waendelee kumuenzi Dkt. Mengi.

Amesema kuwa Dkt. Mengi alikuwa mwenyekiti wa chama hicho(MOAT) tangu kuanzishwa kwake hivyo wataendeleza mshikamano aliouacha.

Ikumbukwe kuwa Dkt. Mengi ambaye alikuwa mmiliki wa vyombo vya habari kadhaa ikiwemo radio one, itv, Magazeti na zingine zilizopo chini ya IPP alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2 Dubai, Falme za kiarabu akiwa matibabuni.

No comments:

Post a comment