Thursday, 2 May 2019

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU WAKATI CHANGAMOTO ZAO ZIKISHUGHULIKIWA


Serikali ya awamu ya tano ni sikivu itashughulikia changamoto za wafanyakazi kote nchini hivyo wawe na subra wakati serikali ikiendelea kuzifanyiakazi na wafanyakazi wafuate wajibu wao.
Akijibu changamoto za wafanyakazi iliyowasilishwa kwenye risala yao kwa Kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha  Idd Kimata kwenye kilele cha siku yao katika uwanja Wa sheikh Amri Abeid amewataka viongozi Wa vyama vya wafanyakazi kupeleka matatizo ya wafanyakazi katika ofisi husika za serikali ili kuzungumzia changamoto mbalimbali za wafanyakazi.
Alibainisha kuwa  serikali aitamfumbia macho mwajiri yeyote Wa sekta binafsi ambaye anamnyanyasa mfanyakazi,na iwapo  itabainika kunamwajiri anaemnyanyasa mfanyakazi basi hatua Kali itachukuliwa thidi take.

“Kunawaajiri ambao wanawanyayasa wafanyakazi nimesikia wanawatolea maneno machafu ,wanawapiga ,na wengine hata kuwanyima haki zao sasa nasema viongozi Wa wafanyakazi naomba muwachukulie hatua na sio ivyo tu iwapo mtambaini mwajiri  yeyote ambaye anawanyayasa wafanyakazi leteni taarifa ili tuwachukulie hatua Kali” alisema kamanta.

Aidha alifafanua kuwa  wiki mbili zijazo uzinduaji wa kiwanda cha matairi general trye serikali itaanza mchakato huo na maagizo ya kuvifuatilia viwanda vingine bilivuofugwa  unaendelea hivyo sherehe za mei mosi sio siku za kuleta changamoto bali ziwe ni furaha.

“Tukae pamoja kabla ya sherehe tuzungumze mapema na tusingoje hadi wakati sherehe hizi za wafanyakazi ndio tunaleta changamoto haileti Afya kwani sherehe ni furaha na milango ipo wazi kutatua kabla ya sherehe”alisema kimanta 
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi Mwenyekiti Wa chama cha waalimu mkoa Wa Arusha Lootha Laizer aliomba serikali kuwachukulia hatua Kali waachiri wote ambao wanawanyanyasa wafanyakazi.

Alisema kumekuwepo na baadhi ya waajiri Wa sekta binafsi wamekuwa na tabia yakuwanyanyasa wafanyakazi kwa kwa kiwapiga ,kuwatolea lugha za matusi na hata kuwanyima haki zao hawa keteni taarifa zao ili tuhangaike nao hili haliwezekani ila mazungumzo ya Mara kwa mara ni sehemu nzuri ya kutatua kero.

Alisema risala mbele ya mgeni rasmi mratibu Wa wafanyakazi mkoa Wa Arusha  Samweli Maghero  aliomba serikali kupunguza kodi ya mapato kwa wafanyakazi kwa ni kodi nikubwa na mshahara ni Mdogo ukilinganisha na hali ya uchumi.

Aidha pia waliomba serikali kupandisha madaraja (vyeo)kwa ni wamekaa kwa kipindi kirefu bila kupandishwa vyeo ,huku aliomba pia serikali iwape ruhusa ya walimu kuhama kwa ni zuhio LA kutohama kwa walimu linawaumiza sana.

No comments:

Post a comment