Thursday, 2 May 2019

UBA YAADHIMISHA MIAKA 70 YA UTUMISHI

Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya United Bank for Africa, Tony Elumelu, akifurahia jambo na washiriki wengine kwenye sherehe ya miaka 70 ya utoaji huduma kwa benki hiyo kwa nchi zaidi ya 50 za Afrika. Sherehe hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini  Lagos nchini Nigeria
LAGOS, NIGERIA
BENKI ya United Bank of Africa (UBA) imeadhimisha miaka 70 tangu ianze kutoa huduma za kibenki kwa wateja wake wakati wa sherehe zilizoongozwa na Mwenyekiti wa kundi la kampuni Tony O. Elumelu.

Sherehe hizo zilizohudhuriwa na wateja, wafanyakazi na marafiki pia zilienda sambamba na hafla ya utoaji Tuzo za kila mwaka za Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO).

Tuzo hizo zilitolewa mbele ya maelfu ya wageni kwa wafanyakazi wa UBA kutoka nchi zote 23 ambako inaendesha shughuli zake kutokana na utendaji wao uliotukuka wa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Miongoni mwa watu mashuhuhuri katika usiku huo pamoja na makadhi, magavana wa zamani na sasa wa majimbo mbalimbali ya Nigeria. 

Aidha marais wa zamani Olusegun Obasanjo na Ibrahim Babaginda, ambao walishindwa kuhudhuria kutokana na dharura walituma barua za kuipongeza benki hiyo kwa ufanisi na mafanikio makubwa yaliyopatikana.

Mwenyekiti wa UBA Plc, Tony Elumelu, ambaye aliambatana na mkewe Dk. Awele, alisema UBA imebakia kuwa taasisi ya kifedha inayoongoza barani Afrika na kutimiza kwake miaka 70 ni mafanikio makubwa.

Alisema, “Huu ni wakati wa kusherehekea urithi tajiri wa kipindi cha miaka mingi na kumwambia kila mtu aliyechangia kile kinachoifanya UBA isimame imara leo hii, kuwa tunashukuru kwa yote na jinsi walivyohakikisha uwekezaji uliowekwa katika benki kipindi cha miongo iliyopita unalipa.” 


Shukrani kama hizo zilitolewa pia na CEO wa Kundi la Kampuni, Kennedy Uzoka huku Mwenyekiti wa Benki ya Zenith, Jim Ovia, akiisifu menejimeni na wafanyakazi wa UBA kwa kuifikisha hapo ilipo.

Ovia alisema; “ UBA inabakia kuwa moja ya benki kubwa kabisa Kusini mwa Sahara Afrika. UBA imeanzishwa kwa ajili ya kudumu. Nawapongeza wafanyakazi wote na wanahisa. Najuta kutonunua hisa za UBA, lakini nadhani sijachelewa kufanya hivyo.
Mwisho

No comments:

Post a comment