Mkuu wa Kampuni ya Benki ya UBA Tanzania, Mussa Kitambi,  akipokea hati ya kutambuliwa kutoka kwa Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa, baada ya benki hiyo kusaidia futari kwa ajili ya watoto yatima 320 wa vituo sita vya Mkoa wa Dar es Salaam. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Afrika.
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya UBA Tanzania, Brendansia Kileo (wa pili wa kulia), akiwa na  amembeba mtoto wa kituo kimojawapo cha yatima jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Afrika.
 Wafanyakazi wa Benki ya UBA Tanzania, wakiwa katika mavazi ya kiasili ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kumbukumbu ya nchi huru za Afrika
Wanyakazi wa Benki ya UBA Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe za wiki ya Afrika

 Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
BENKI ya UBA Tanzania imeungana na nchi zingine za Afrika kwa kushehereke siku ya Afrika kama sehemu ya kumbukumbuku ya kila mwaka ya kuanzishwa kwa OAU na sasa AU ambao ulianzishwa Mei 25, mwaka 1963
Kwa hapa nchini benki hiyo iliadhimisha siku hiyo UBA Tanzania,  iliadhimisha siku hiyo kwa wafanyakazi wake kuvaa ngu za mitindo mbalimbali yenye kuonyesha uhalisia wa waafrika.
Akizungumzia siku hiyo Mkuu wa Kampuni ya Benki ya UBA Tanzania, Mussa Kitambi, alisema kuasisiwa kwa benki hiyo kunajumuisha historia ya Afrika kupitia mavazi, umoja na vyakula vya jadi.
“Siku ya Afrika (zamani ya Uhuru wa Afrika na Siku ya Uhuru wa Afrika) ni kumbukumbu ya kila mwaka ya msingi wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) inayojulikana kama Umoja wa Afrika mnamo 25 Mei 1963. Inaadhimishwa katika nchi mbalimbali katika bara la Afrika , pamoja na duniani kote,” alisema Kitambi 
Katika kukumbuka siku hiyo shughuli mbalimbali zilifanyika kuvunja nazi, kukata keki na wateja, ngoma ya jadi na wafanyakazi, ngoma ya jadi na kikundi cha flash.
MWISHO
Share To:

Post A Comment: