Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua kikao cha
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya
Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

 Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akitoa taarifa
ya utangulizi kwenye ufunguzi wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya ugatuaji wa
madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Baadhi wa Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-
TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu
ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi
wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

 Baadhi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi
OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia
rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika
ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya
pamoja na Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia
Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa
mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya
pamoja na Makatibu Tawala mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia
Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa
mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Kutokuwepo kwa Sera ya Ugatuaji Madaraka iliyojengwa kwenye mfumo
wa Sheria ni moja ya changamoto iliyofanya Serikali kufanya mapitio ya
sera hiyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo(Mb) wakati wa kufungua kikoa kazi
kilichokutanisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutoka
Mikoa yote 26 kwa ajili ya kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu
ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka ya 2019.

Alisema kuwa changamoto moja wapo ni kutokuwepo kwa sera ya ugatuaji
iliyojengwa kwenye mfumo wa kisheria inayoelekeza mipaka, majukumu na
utaratibu wa utekelezaji wake, jambo ambalo linafanya ionekane kama ni
hiari na utashi (Voluntary and Willingness).

Jafo alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa mitazamo inayokinzana
kati ya watendaji na viongozi wa kisiasa katika ngazi ya vijiji, kata na
halmashauri katika kuweka vipaumbele na kutekeleza miradi ya maendeleo
Aliongeza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitegemea fedha
kwa kiasi kikubwa kutoka Serikali kuu na kutolea mfano kwa mwaka 2018
zilitegemea zaidi ya asilimia 88 ya mapato.

“ Wizara za Kisekta kuandaa sera na sheria na kupeleka halmashauri kwa
ajili ya utekelezaji bila kuambatanisha rasilimali fedha, vifaa na watu.”
Waziri Jafo alibainisha kuwa uelewa mdogo wa dhana ya Ugatuaji wa
Madaraka (D by D) kwa baadhi ya Wizara za Kisekta na hivyo Sera hii
kuonekana kama ni suala ya OR-TAMISEMI kwa kiasi kikubwa
imechangia kufanya Sera hii kutotekelezeka kwa kiwango
kilichotegemewa.

Jafo aliongeza: “Kwa ujumla hatujafikia kiwango cha mafanikio
kilichotarajiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeaza na ndio

maana Serikali imeamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji ili
kupata suluhisho la changamoto zilizojitokea.
Aidha, Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuhakikisha
wanashiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo hayo ili
kuboresha rasimu hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi, wadau na taifa
kwa ujumla.
Aidha Mhe. Jafo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakuu wa mikoa na
makatibu tawala wa mikoa kuhakikisha wanasimamia kwa ukabilifu fedha
na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya,
ujenzi wa hospitali za wilata, ujenzi wa mabweni, madarasa, vyoo katika
shule za msingi na sekondari ambayo tayari fedha zake zimeshatolewa na
serikali.

Naye Mwenyekiti wa wakuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Eng. Evarist Ndikilo aliahidi kushiriki mzuri wa wawakuu hao kwa
kuwa wao ndio wanaotoka kwa wananchi.
Pia alimhakikishia Waziri Jafo kuwa watasimamia kwa umakini utekelezaji
wa miradi ya maendeleo na kuwa itakamilika katika muda uliopangwa na
kwa ubora unaotakiwa.

Naye Mwakilishi wa UNICEF, Pius Chaya alisema agenda ya mapitio ya
Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka imekuja wakati muafaka, kwasababu
Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma
wanazostahili na ambazo zinawafikia kwa wakati.

Aidha, Chaya alisema wadau wa maendeo ambao pia wameshiriki katika
machakto wa mapitio ya sera hiyo wameahidi kuendelea kushirikiana na
serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo
Sera ya Ugatuaji wa Madaraka ni dhana ya Kupeleka Madaraka,
Majukumu na Rasilimali kutoka Serikali Kuu kwenda kwa Wananchi kupitia
vyombo vya kidemokrasia na Kisiasa ambavyo, wajumbe wake
huchaguliwa na kuwajibika kwa Wananchi na vimepewa Mamlaka ya kutoa
Maamuzi na kusimamia rasilimali (yaani vina uhuru, vinajitawala, na vina
hadhi ya kisheria).

Sera hii ilianza kutekelezwa mwaka 1998 kupitia mpango wa maboresho
ya Serikali za Mitaa ikiwa na lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki
shughuli za Maendeleo katika maeneo yao na kuongeza ufanisi katika
uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: