Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Mwakili wa UNICEF
Tanzania Bi. Maniza Zaman alipokwenda kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa
kufanya kazi nchini Mei 10, 2019 Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman (kulia)
akimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.
Anthony Mavunde. (katikati) ni Bi. Khadija Othman
mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi.
Maniza Zaman,
akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde alipomtembelea Ofisini kwake
Jijini Dodoma. (Kulia) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akioneshwa picha ya Watoto na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada
ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo Mwakilishi wa UNICEF
Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili
jambo na Mkuu
wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kulia), (katikati) ni
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii Bw. Daud Kaali.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE
ULEMAVU)
Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amekutana
na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Bi.
Maniza Zaman ambaye amemaliza muda wake alipomtembelea Ofisi kwake iliyopo Jijini
Dodoma.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Mavunde amelipongeza Shirika
la Umoja wa Mataifa la UNICEF kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea
wananchi maendeleo na kwa kutoa misaada katika sekta mbalimbali nchini.
“UNICEF imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Waziri
Mkuu katika masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security
Policy of 2003), kuwapatia mafunzo watumishi katika masuala ya virutubishi
na hifadhi ya jamii, pia kuwapatia vitendea kazi kama vile komputa na magari
ambayo yanatumika kwenye miradi mbalimbali,” alieleza Mavunde.
Aliongeza kuwa, Serikali imeguswa na jitihada za
UNICEF na itaendeleza ushirikiano na shirika hilo katika kutekeleza jukumu la
kuhudumia Watoto.
Aidha, Naibu Waziri Mavunde alimpongeza Bi. Maniza Zaman kwa kazi nzuri aliyofanya kipindi cha
muda wake na kumsihi kuendelea kuwa balozi mzuri wa masuala ya Watoto.
“Tutakukumbuka kwa juhudi na ushauri uliokuwa
ukitupatia katika masuala ya elimu na haki za Watoto,” alisema Mavunde.
Kwa upande wake, Bi. Maniza Zaman amesema
anaishukuru Serikali kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa
hapa nchini.
MWISHO
Post A Comment: