Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma leo Jumatatu Mei 6, wakati akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea.
 
Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema hawajapata taarifa rasmi kwanini mbunge huyo amekamatwa.

“Huu ni mwendelezo wa matukio ya viongozi wetu kukamatwa, licha kwamba walitakiwa kuujulisha uongozi wa bunge,” amesema Silinde.

Alipoulizwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hana taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo.

"Niko Gairo sijapata taarifa zozote za  kukamatwa kwa mbunge huyo," amesema Muroto.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: