Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani
Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na
Kyela mkoani humo ambapo IGP Sirro aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akinunua matunda kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali katika eneo la
Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika
wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo kwa lengo la kuona utendajikazi
unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha
na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajasiliamali ndogo ndogo katika eneo
la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, IGP Sirro yupo mkoani hapa kwa ziara ya
kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa ajili yake wakati alipowasili katika Kituo
Kikuu cha Polisi wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo
la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia Kitta, wakati
alipowasilia wilayani humo kwa ziara ya kikazi yeye lengo la kuona utendajikazi
unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha
na Jeshi la Polisi.
Post A Comment: