Na Rahel Nyabali, Tabora

Ili kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama nchini wadau binafsi Mkoani Tabora wametakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuchangia ujenzi wa Nyumba za Askari Polisi ziweze kukamilika katika ubora unaotakiwa, hatua ambayo itasaidia kuvutia wawekezaji mbalimbali kuwekeza nchini.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoani Tabora kamishna msaidizi Emmanuel Nley amesema jeshi hilo linaupungufu wa zaidi ya shilingi milioni themanini na nne ambazo zinahitajika katika ujenzi wa Nyumba hizo.

“Nyumba hizi zitajengwa katika mfumo wa mbili kwa moja yenye na gharama halisi ya kila nyumba moja ni zaidi ya shilingi milioni miabili hamsini na nne tunawaomba wadau kuniunga mkono kukamilisha ujenzi wa nyumba hizi” Amesema Nley.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ambaye amekuwa mgeni Rasmi katika halambee  iliyowakutanisha wadau wa maenedeleo wilayani Tabora mkoni Tabora amesema  lengo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuchangia nyumba za Askari polisi.

“Tukijipanga vizuri hapa tuna jeshi la polisi, jeshi la Magereza, tunavijana wazuli wa jeshi la wananchi JWZ, bodaboda tukiamua kujenga kwa umoja tutatoka hapa tulipo” Amesema Mwanri.

Aidha ametoa rai katika matumizi ya fedha hizo zitakazo tumika katika ujenzi kufanya kazi husika ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa viwango sitahiki.

“Hela hii haita liwa hawa watu ndio wanaosukuma ndani wakitumia fhedha hii kinyume na ujenzi wa nyumba hizi watasukumwa ndani wao” amesema Mwanri
Share To:

msumbanews

Post A Comment: