Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(kushoto) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi
Adesina, Mjini Washington DC, Marekani, kabla ya mkutano wa magavana wa Benki
hiyo ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 zenye hisa kwenye benki uliofanyika
katika ukumbi wa Willard Continental kujadili namna ya benki hiyo kuongezewa
mtaji ili iweze kutoa mikopo kwenye nchi hizo kwa ufanisi zaidi
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki
ya Maendeleo ya Afrika-AfDB inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC,
Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(kulia) akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo
Tanzania imeridhia hatua hiyo
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha
na Mipango-Washington DC
Benny Mwaipaja, WFM,
Washington DC
TANZANIA imeunga mkono
uamuzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB wa kutaka kuongezewa mtaji ili
iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa mikopo kwa nchi wanachama wa benki hiyo
kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akizungumza baada ya
kumalizika kwa mkutano wa 7 wa magavana wa ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka
nchi 54 wanachama wa Benki hiyo, Mjini
Washington DC, Marekani, Waziri wa Fedfha na Mipango, Dkt. Philip Mpango
ameeleza kuwa AfDB imefanya mambo makubwa nchini Tanzania ndio sababu inaunga
mkono kusudio hilo.
Amesema kuwa Benki hiyo
imeipatia Tanzania mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa
ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, kilimo, nishati na maji.
Benki inataka kuongezewa
mtaji kwa asilimia 200 kutoka wastani wa UA bilioni 67.69 hadi UA 191.89
(kutoka dola za Marekani 94.76 hadi dola bilioni 268.6 ili kuchochea mageuzi ya
kiuchumi na kijamii ya nchi wanachama hususan katika ujenzi wa reli, barabara,
usafiri wa anga, tehama, bandari, uzalishaji na usambazaji wa nishati.
"Wakati umefika ili
twende haraka zaidi, mitaji sehemu nyingine imepungua, pendekezo la kuongeza
mtaji wa benki hii ni jema na matokeo ya miradi inayofadhiliwa na Benki hii yanaonekana
katika nchi zetu za kiafrika kwa sababu benki hii iko Afrika na inaijua Afrika
tofauti na benki nyingine" alisisitiza Dkt. Mpango
Uamuzi wa nchi za Kiafrika
zenye hisa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika ya kutaka Benki hiyo iongezewe
mtaji ulitolewa wakati wa mkutano wa Magavana wa Benki hiyo mjini Rome, Italia,
baada ya mahitaji ya nchi wanachama ya kutafuta mikopo kwenye taasisi hiyo
kuongezeka.
Mwisho
Post A Comment: