Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu wake Anthony Mavunde (wa kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Andrew Massawe wakitembea katika viwanja vya Bustani ya Jiji wakati wa kukagua mabanda ya maonesho katika kuadhimisha Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Aprili 28, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.

Waziri Jenista Mhagama akipokelewa na watumishi wa OSHA alipowasili katika viwanja vya bustani ya Jiji Mkoani Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika mkoani hapo kitaifa.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Khadija Mwenda akieleza jambo kwa Waziri Jenista Mhagama wakati wa maaadhimisho hayo, wa kwanza kushoto ni Naibu wake Anthony Mavunde.

Mhe.Jenista Mhagama akipewa maelezo ya vifaa saidizi kazini kutoka kwa Mtaalamu kutoka Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri Jenista Mhagama akiuliza jambo kwa wataalam kutoka Idara ya Kazi wa ofisi hiyo alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Stella Ikupa akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la maonesho la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri wa Nchi, Jenista pamoja na Naibu wake Anthony Mavunde wakiangalia mfano wa namna ya kuokoa mtu aliyepata madhara awapo kazini walipotembelea banda la MUST (Mbeya University of Science and Technology) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Jijini Mbeya.

Waziri Jenista pamoja na baadhi ya viongozi wa TUGHE wakifurahia jambo wakati alipotembelea banda la TUGHE katika maonesho hayo.

Mhe.Jenista akifuatilia takwimu za ajari zitokananazo na shughuli za uchimbaji katika Mgodi wa Dhahabu waBulyanhulu alipotembelea banda la ofisi hiyo kujionea namna wanavyofanya kazi wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Mkoani Mbeya.

Waziri Jenista akihutubia wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya kilele maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya Aprili 28, 2019.

Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Jenista (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya.

Jenista akifurahia pamoja na watumishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM) baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kupokea tuzo nyingi kuliko washiriki wengine wa maonesho ya Siku Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya.
Share To:

Post A Comment: