Wednesday, 24 April 2019

RAIS MAGUFULI AWASILI MALAWI KIKAZI


Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 24 Aprili, 2019 ameondoka hapa nchini kwenda nchini Malawi ambako anafanya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku 2 kwamwaliko wa Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika.
Dtk. Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na atapokelewa rasmi na mwenyeji wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu Mjini Lilongwe.
Akiwa Mjini Lilongwe Rais Magufuli ataweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Malawi Hayati Bingu Mutharika, kasha atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Mutharika, na jioni atahudhuria Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais Mutharika.
Kesho Magufuli akiwa na mwenyeji wake  Rais Mutharika atamaliza ziara yake kwa kufungua msimu wa Soko la Tumbaku na kuzungumza na wadau wa zao hilo na baadaye atarejea nchini Tanzania ambako ataanza ziara ya kikazi ya siku 8 Mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment