Tuesday, 2 April 2019

MUHEZA UNITED MABINGWA WA KOMBE LA ADADI CUP MUHEZA

 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi ya Adadi Cup nahodha wa timu ya Muheza United ambao ndio mabingwa wapya wa mashindano hayo halfa hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo
  MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi ya Adadi Cup nahodha wa timu ya Muheza United ambao ndio mabingwa wapya wa mashindano hayo halfa hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo
  MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akimkabidhi zawadi za Jezi  nahodha wa timu ya Muheza United ambao ndio mabingwa wapya wa mashindano ya Adadi Cup  halfa hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo
Kocha wa timu ya Muheza United ambao ndio mabingwa wapya wa Kombe la Adadi Cup wakiwa wamembeba juu mara baada ya kuibuka na ushindi wa kombe hilo

TIMU ya soka ya Muheza United  wamefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Adadi Cup baada ya kuibamiza Watu Pori mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza.

Ubingwa huo umewafanya Muheza United kujinyakulia Ng’ombe, kitita cha laki tano,jezi seti moja,mpira mmoja na kikimbe cha mashindano hayo kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu.

Mshindi wa pili kwenye mashindano hayo ilikwenda kwa Chama la Wana ambao walijinyakulia mbuzi mmoja, kitita cha laki tatu, mpira mmoja na jezi seti moja.

Nafasi ya mshindi wa tatu akijinyakulia kitita cha sh.laki moja,jezi seti moja na mpira mmoja huku mfungaji bora ,kipa bora,timu bora na mchezaji bora wakiondoka na kitita cha elfu arobaini kila mmoja wakati mwamuzi bora akipata elfu hamsini.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi, Mbunge Balozi Adadi alisema baada ya kumalizika mashindano hayo anarudi kujipanga tena kuhakikisha ligi hiyo inaendelea kuchezwa ili kuweza kuibua vipaji vya wachezaji kutoka kwenye tarafa zote.

Alisema lengo lake ni kuhakikisha siku zinazokuja wilaya hiyo iweze kuwa na wachezaji wengi wazuri ambao watauzwa kwenye maeneo mbalimbali hususani kwenye timu kongwe hapa nchini.

Mwisho.

No comments:

Post a comment