Saturday, 13 April 2019

Mch. Msigwa adai bendera za Chadema hushushwa akipita Rais MagufuliMbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mch. Peter Msigwa amesema mahali popote ambako Rais Magufuli hupita bendera za Chadema hushushwa na kuwekwa za CCM.

“Siku za hivi karibuni kumezuka tabia ambayo inakiuka na haitambui kuwa nchi yetu ni ya vyama vingi,”Mchungaji Msigwa ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma baada ya kuomba mwongozo.

“Mahali popote ambako Rais anapita bendera za Chadema zinashushwa hadi katika ofisi za chama. Mfano Mafinga zimeng’olewa barabarani na kuwekwa za CCM.  Iringa mjini bendera za CCM zimewekwa hadi kwenye mistimu,” amesema.

Mbunge huyo amedai kitendo hicho kinafanyika katika nchi yenye  mfumo wa vyama vingi jambo alilodai kuwa linachochea vurugu na chuki kati  ya Watanzania.

No comments:

Post a comment