NA HERI SHAABAN
MANISPAA ya Ilala imetoa mafunzo kwa Askari Mgambo wa Manispaa hiyo wanaosimamia masuala ya usafi wakiwataka wafanye kazi kwa weledi.


Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Ilala Abdom Mapunda alipokuwa akizungumza na mgambo wake na kuwaeleza mikakati ya kazi .

"Mgambo wangu nawaomba mfanye kazi kwa weledi muepuke kuchukua rushwa   simamieni misingi ya kazi  na kufuata kanuni za kazi "alisema Mapunda.


Mapunda alisema   manispaa hiyo imewaboreshea maslahi yao ya kazi kuanzia sasa hivyo wafanye kazi na kufuata misingi ya kazi wanalipwa kwa wakati.


Aidha aliwataka Mgambo  kufanya kazi iliowaleta  kwani Ilala ndio sura ya nchi wasitie doa manispaa hiyo.

Aliwapongeza kwa kufanya kazi vizuri na kuwaagiza   wawachukulie hatua Askari Mgambo feki ambao wanajifanya  wapo Manispaa Ilala.


Mapunda alisema mgambo wake wote waliopo Ilala wanaosimamia usafi wapo zaidi ya 100 na vitambulisho maalum vitavyowatambulisha kazi hiyo.


"Katika kipindi cha Mwaka mmoja eneo la katikati ya jiji mgambo hao wamesimamia suala la usafi vizuri kwa kutoa Elimu kwa wananchi sambamba na kuwakamata wachafuzi wa mazingira"alisema

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: