Polisi mkoani Tanga wamewaua watu watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliotaka kuvamia na kupora mishahara ya wafanyakazi katika shamba la mkonge la Toronto wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu saa 2:00 usiku kwenye eneo hilo ambako majambazi hayo yaligundua siku hiyo wafanyakazi wangelipwa mishahara  yalikwenda kuvamia na kutaka kupora fedha hizo.

Katika tukio hilo, mkuu wa upepelezi wilaya ya Korogwe, Samson Mwandambo, alipigwa risasi kufuani lakini kwa sababu alikuwa amevaa koti la kuzuia risasi (buleti Proof ) lilimsaidia risasi kutopenya hadi mwilini mwake.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Edward Bukombe, amesema baada ya askari kupata taarifa hizo  walifuatilia na majambazi hayo yalipoona hali hiyo yalianza kurushiana risasi na askari kwa saa kadhaa.

Akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa, Bukombe amesema majambazi hayo yalianza mapambano na askari kuanzia eneo la Mombo mpaka eneo la Toronto wilayani hapa.

Amesema katika majibizano hayo ya risasi, polisi waliwapiga risasi majambazi hayo na kuwadhibiti.

Kamanda huyo amesema baada ya kumalizika kwa majibizano hayo ya risasi,  polisi waliyaua majambazi hayo  na kukuta bunduki mbili aina ya Shotgun kwenye eneo la tukio na bastola ambazo zilikuwa na risasi tano na maganda matatu ya risasi ambayo walirushiana na askari eneo hilo.

Amesema miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga, kwa ajili ya taratibu nyengine.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: